Tazama Pichaz za kikongwe anayedhaniwa kuwa mchawi alivyokamatwa chumbani kwa mtu akiwa mtupu Mjini Bukoba. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 02, 2014

Tazama Pichaz za kikongwe anayedhaniwa kuwa mchawi alivyokamatwa chumbani kwa mtu akiwa mtupu Mjini Bukoba.

Hili ni tukio lilitokea Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, ambalo linamhusisha Kikongwe mmoja ambaye jina lake bado halijapatikana kukutwa chumbani kwa mtu huku akiwa mtupu chumbani kwa mtu alfajiri ya January 31,2014.


Mpaka sasa bado haijajulikana kama ni Kigarura au pengine alipata matamani ya mwili akaona pengine chumba kile kingemfaa kumpatia msaada wa mambo yake.

Bibi Kizee huyo anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 70,ambapo amekamatwa alfajiri ya  January 31,2014, hata hivyo polisi wamefanikiwa kumnusuru na kifo baada ya kumchukua na kumpeleka kituo cha polisi.

Mashuhuda wa mwanzo wanadai walimkuta bibi huyo akitapatapa bila kujua nini la kufanya huku akiwa mtupu na nguo zake zikiwa pembeni kitendo kilichotafsiriwa kwamba pengine bibi huyo anaweza kuwa mchawi,huku wengine wakisubiri taarifa ya polisi na wengine wakisema huenda bibi huyo alipatwa na matamanio ya kimwili.
Habari Na picha:-Bukobawadaublog.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad