![]() |
|
Muonekano wa
gari aina ya Toyota Corolla T 770 ABT likiwa limeharibika vibaya likiwa kituo cha Polisi Dodoma.
|
Askari
polisi watano mkoani dodoma wamefariki dunia papo hapo katika ajali ya gari
iliyotokea 31/01/2014 majira ya saa 5 usiku katika barabara kuu ya Dodoma –
Morogoro eneo la Mtumba Center, Kata ya Mtumba Tarafa ya Kikombo Manispaa ya
Dodoma, ambapo gari namba ya usajili
T.770 ABT Toyota Corolla lililokuwa likiendeshwa na Askari mwenye namba H. 3783
PC DEOGRATIUS wa Wilaya ya Kongwa.
Gari hilo
lilikuwa likitokea Dodoma mjini likielekea Wilayani Kongwa liligongana uso kwa
uso na gari namba T.997AVW Scania Bus mali ya Kampuni ya Mohamed Trans
lililokuwa likiendeshwa na JUMA s/o MOHAMED, miaka 38, Mkazi wa Mwanza,
likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma na kusababisha vifo kwa askari watano
papo hapo.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME
amewataja Askari hao waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni:-
1. D.9084 D/CPL. ADOLF S/O MESHACK SILLA mwenye
miaka 51, Mgogo.
2. F.6459 D/C. EVARIST s/o MOSES BUKOMBE mwenye
miaka 34, Muha.
3. H.3783
PC. DEOGRATIUS s/o PATRICK MAHINYILA mwenyw miaka 29, Mgogo.
4. WP.10337
PC. JACKLINE d/o AUGUSTINE TESHA mwenye miaka 22, Mchaga.
5. WP.10382 PC. JEMA d/o JIMMY LUVINGA mwenye
miaka 20, Mhehe.
Wote ni
askari Polisi Wilaya ya Kongwa na hakuna abiria aliyeumia katika basi.
Dereva wa Bus alitoroka mara baada ya ajali hiyo kutokea, juhudi za kumtafuta zinaendelea.
Miili ya marehemu imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya mkoa Dodoma.
Aidha
Kamanda MISIME ametoa wito kwa madereva kila mara wawe na udereva wa tahadhari
na na kuzingatia sheria za usalama barabarani.



.jpg)
.jpg)




No comments:
Post a Comment