Muonekano wa Ndani ya ukumbi huo baada ya kazi ya uwekaji viti
kukamilika.
|
Mojawapo ya viti maalum vilivyowekwea katika ukumbi huo kwa ajili ya
matumizi ya watu wenye ulemavu, kwa ajiri ya matumizi ya Bunge la Katiba.
|
Viti vyote vipya vina nembo ya taifa,ukumbi wa Bunge kwa ajiri ya
matumizi ya Bunge la Katiba.
|
Tayari Serikali ya Tanzania imetangaza majina ya wajumbe walioteuliwa
kushiriki bunge la katiba linalotarajiwa kuanza tarehe 18 ya mwezi huu mjini
Dodoma.
Majina hayo yametangazwa ijumaa Februari 07,2014 jioni na Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Florence Turuka mbele ya
waandishi wa habari ikulu jijini Dar es salaam.
Wajumbe wa
bunge ni Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi la Zanzibar na Wajumbe 201 walioorodheshwa kwa mujibu wa Kifungu
Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi
mbalimbali 10 yanayohusika.
Majina hayo
yametangazwa siku moja toka Rais wa nchi hiyo Jakaya Mrisho kikwete kuwaonya
watakaoteuliwa kusimamia maslahi ya Taifa na kuweka kando itikadi zao.
Akizungumza
katika kikao cha Baraza la Vyama vya siasa siku ya alhamisi jijini Dar es
salaam, Rais Kikwete alisema Watanzania wanatarajia kuona mchakato huo
ukiendeshwa kwa amani na utulivu hivyo wajumbe wote na vyama vya siasa
watangulize mbele maslahi ya Taifa badala ya kuweka mbele maslahi binafsi au ya
vyama vyao.
Baadhi ya
majina yaliyoingia ni Prof. Ibrahim Lipumba, prof. Abdalah Safari , Paul
kimiti, Kingunge Ngombale Mwiru, Peter Kuga mziray, Christoper Mtikila, John
Lifa Chipaka, Emmanuel Makaidi ,Godfrey Simbeye, Kajubi Mukajaga, Paul Makonda
na Julius Itatiro.
Bunge la
katiba litakutana kwa siku 70 na huenda likaongezewa siku 20 zaidi endapo
hakutakuwa na maafikiano ili kujadili rasimu ya pili ya katiba iliyotolewa na
Tume ya Mabadiliko ya Katiba mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment