Akitoa shukrani hizo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
amesema leo (Feb 10,2014) kwamba siri ya CCM kuimwaga CHADEMA ni uadilifu katika kuwatumikia
wananchi na kwamba, kushindwa kwa chama hicho ni ushahidi kwamba hakikubaliki
na Watanzania wamewathibitishia kwamba hawajazoea vurugu.
Nape alisema CCM inaahidi kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa amani na
utulivu kwa kuwa ina uzoefu wa kufanya siasa kistaarabu na ndio siri ya
kukubalika kwa wananchi.
Akizungumzia kushindwa kwa CHADEMA alisema wamehukumiwa kutokana na
vurugu na kupiga watu kwenye kampeni za uchaguzi na ndio maana wametumia
gharama kubwa na helkopta tatu na kuambulia kata tatu.
"CHADEMA wamevuna walichopanda Watanzania hawapenda vurugu, wamezoea
amani na utulivu sasa wamewaadhibu kwa kuwanyima kura na huo ni ushahidi kwamba
Watanzania hawakiamini," alisema.
Katika uchaguzi huo CCM ilishinda katika kata CCM ilishinda katika kata
23 za Kibindu na Magomeni (Pwani), Kiwalala na Namikage (Lindi), Ubwage
(Shinyanga), Ibumu na Nduli (Iringa), Kiomoni na Mtae (Tanga),
Nyasura(Mara), Malindo, Santillya (Mbeya), Partimbo(Arusha, Mkwiti (Mtwara),
Tungi na Ludewa (Morogoro) na Mrijo (Dodoma).
No comments:
Post a Comment