Tazama Goli la Dakika za Majeruhi kwa Chelsea,Arsenal ,Manchester City na United wakishinda mechi zao za Ligi Kuu Uingereza huku FC Barcelona wakichapwa 3-1 na kuwabakisha Real Madrid kileleni mwa Ligi ya Hispania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 23, 2014

Tazama Goli la Dakika za Majeruhi kwa Chelsea,Arsenal ,Manchester City na United wakishinda mechi zao za Ligi Kuu Uingereza huku FC Barcelona wakichapwa 3-1 na kuwabakisha Real Madrid kileleni mwa Ligi ya Hispania.

John Terry alikuwa wa kwanza kuugusa mpira huku Slyvain Distin, Leighton Baines na Phil Jagielka wa Everton wakiangalia walipofungwa na  Chelsea  Bao  1-0 , Ushindi huu umewafanya Chelsea waendelee kudumisha Rekodi yao ya kutofungwa na Everton Uwanjani Stamford katika Mechi za Ligi Kuu na Rekodi inasimama kwa Ushindi Mechi 10 na Sare 9. 
Goli la Dakika za Majeruhi Jana februari 22,2014 ,mchana  huko Stamford Bridge limewapa Chelsea ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na Everton na kuwawezesha kuendelea kukaa kileleni mwa Ligi Kuu Uingereza wakiwa Pointi 1 mbele ya Arsenal.

Bao hilo lilifungwa baada ya Frank Lampard kupiga Frikiki ambayo John Terry aliitokea na kumletea kashikashi Kipa Tim Howard bila kugusa Mpira na shuti hilo la Lampard kumgonga Howard mkononi na kutiririka wavuni.

Hili lilikuwa pigo la kikatili kwa Everton ambao katika Mecho nzima walisimama kidete kuikabili Chelsea huku Kipa wao Tim Howard akisimama imara kuzuia majaribio ya Samuel Eto'o, Eden Hazard, Lampard na Branislav Ivanovic.

Ushindi huu umewafanya Chelsea waendelee kudumisha Rekodi yao ya kutofungwa na Everton Uwanjani Stamford katika Mechi za Ligi Kuu na Rekodi inasimama kwa Ushindi Mechi 10 na Sare 9. 


Yaya Toure (juu) akimrukia Aleksander Kolorov mgongoni baada ya kufunga bao pekee la ushindi kwa Manchester City na ikirejea kwenye wimbi la ushindi baada ya kuilaza 1-0 Stoke City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad jana Jumamosi Februari 22,2014 usiku.

Bao la Dakika ya 70 la Yaya Toure alieunganisha Krosi ya Aleksandar Kolarov limewapa Man City ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Stoke City iliyopigana kiume na ushindi huo wa City umekuja baada ya kuadhiriwa na Barcelona katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Matokeo hayo yanafanya City ibaki inazidiwa pointi tatu tu vinara wa Ligi Kuu Chelsea, ingawa kikosi cha Manuel Pellegrini kina mchezo mmoja mkononi.


Mchezaji Laurent Koscielny (katikati) akisherehekea baada ya kufunga goli kwa pamoja na Oliver Giroud (kushoto) na Per Mertesacke pale Timu ya Arsenal kushinda mabao 4-1 dhidi ya Sunderland katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza Jana Februari 22,2014 usiku.

Bao za Mchezaji Olivier Giroud, Bao 2, Tomas Rosicky na Laurent Koscielny ziliwapa Arsenal ushindi wa Bao 4-1 walipocheza na Sunderland Uwanjani Emirates.
Bao pekee la Sunderland lilifungwa na Emanuele Giaccherini.

Ushindi huu umewafanya Arsenal waendelee kukamata Nafasi ya Pili kwenye Ligi Kuu Uingereza wakiwa Pointi 1 nyuma ya Chelsea ambao jana mapema waliifunga Everton Bao 1-0.

Siku moja baada ya kusaini Mkataba mpya wa miaka mitano utakaomfanya awe mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani, Pauni 300,000 kwa wiki, Wayne Rooney amewafurahisha Manchester United kwa kufunga katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace ugenini katika Ligi Kuu ya England jana februari 22,2014 usiku.

Wakicheza Ugenini huko Selhurst Park kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na Timu ngumu ya Crystal Palace, Mabingwa Watetezi wa England, Manchester United, walishinda Bao 2-0 na kujikongoja Nafasi moja juu na sasa kukamata Nafasi ya 6.
Hadi Mapumziko Mabao yalikuwa 0-0.

Kipindi cha Pili, katika Dakika ya 62, Robin van Persie aliipatia Man United Bao la Kwanza kwa Penati iliyotolewa na Refa Michael Oliver baada Patrice Evra kuangushwa ndani ya Boksi na Marouanne Chamakh.

Bao la Pili lilifungwa Dakika ya 68 kifundi na Wayne Rooney baada ya kupokea pasi safi toka kwa Evra.

Mechi inayofuata kwa Man United ni huko Ugiriki hapo Jumanne Usiku watakapocheza na Olympiacos katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.


Matokeo ya EPL Jana Jumamosi Februari 22,2014.

Chelsea 1 Everton 0
Arsenal 4 Sunderland 1
Cardiff 0 Hull 4
Man City 1 Stoke 0
West Brom 1 Fulham 1
West Ham 3 Southampton 1
Crystal Palace 0 Man United 2

Ratiba ya Mechi za leo Jumapili Februari 23,2014.

1630 Liverpool v Swansea
1630 Newcastle v Aston Villa
1900 Norwich v Tottenham


Position Team Played Goal Difference Points
LA LIGA:-HISPANIA-‘’ANOETA’’ ni Uwanja ambao FC Barcelona walikuwa hawajashinda katika Mechi zao 5 zilizopita na Jana Februari 22,2014,Usiku walipata kipondo cha Bao 3-1 kutoka kwa Real Sociedad katika Mechi ya La Liga na kuwabakisha Real Madrid wakiwa kileleni mwa Ligi hiyo ya soka nchini Hispania.

Barcelona, wakitokea kwenye furaha ya kuichapa Manchester City 2-0 huko Etihad katika Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Jumanne iliyopita, walijikuta wako nyuma kwa Bao 1 katika Dakika ya 32 kupitia kichwa cha Gorka Elustondo kilichomgonga Begani Alex Song na kutinga.

Dakika 4 baadae Lionel Messi akaisawazishia Barcelona lakini Bao 2 za Real Sociedad ndani ya Dakika 14 za kwanza za Kipindi cha Pili zilizofungwa na Antoine Griezmann na David Zurutuza, zilihakikisha Barca wanaondoka Uwanjani Anoeta, Mjini San Sebastian mikono mitupu kwa mara ya 3 katika Misimu minne.

Mapema Jana, Real Madrid, ikicheza bila ya Cristiano Ronaldo aliekuwa akimalizia Kifungo chake cha Mechi 3, iliichapa Elche Bao 3-0 kwa Bao za  Asier Illaramendi, Gareth Bale na Isco, na kutwaa uongozi wa La Liga wakiwa Pointi 3 mbele ya Barcelona na Atletico Madrid.

LeoJumapili februari 23,2014, Atletico Madrid wanacheza Ugenini na Osasuna na wakishinda Bao 4-0 watatwaa uongozi wa Ligi.

Matokeo ya La Liga 2013/2014 Ijumaa Februari 21,2014.

Real Valladolid 1 Levante 1

Jumamosi Februari 22,2014.

Real Madrid CF 3 Elche CF 0
Celta de Vigo 1 Getafe CF 1
Real Sociedad 3 FC Barcelona 1
UD Almeria 0 Malaga CF 0

Jumapili Februari 23,2014.

1400 Rayo Vallecano v Sevilla FC
1900 Real Betis v Athletic de Bilbao
2100 Valencia v Granada CF
2300 Osasuna v Atletico de Madrid
2359 RCD Espanyol v Villarreal CF

League Table La Liga 2013/2014.


Position Team Played Goal Difference Points
1 Real Madrid 25 47 63
2 Barcelona 25 50 60
3 Atlético Madrid 24 43 60
4 Athletic Bilbao 24 13 44
5 Real Sociedad 25 11 43
6 Villarreal 24 15 40
7 Levante 25 -7 33
8 Sevilla 24 1 32
9 Valencia CF 24 1 32
10 Espanyol 24 -2 32
11 Celta de Vigo 25 -4 30
12 Granada CF 24 -9 27
13 Elche 25 -15 26
14 Osasuna 24 -16 26
15 Getafe 25 -17 26
16 Almería 25 -18 26
17 Málaga 25 -11 25
18 Real Valladolid 25 -16 22
19 Rayo Vallecano 24 -33 20
20 Real Betis 24 -33 14
1 Chelsea 27 28 60
2 Arsenal 27 25 59
3 Man City 26 42 57
4 Liverpool 26 34 53
5 Tottenham 26 4 50
6 Man Utd 27 12 45
7 Everton 26 10 45
8 Southampton 27 6 39
9 Newcastle 26 -6 37
10 West Ham 27 -3 31
11 Hull 27 -2 30
12 Swansea 26 -3 28
13 Aston Villa 26 -9 28
14 Stoke 27 -15 27
15 Crystal Palace 26 -18 26
16 West Brom 27 -8 25
17 Norwich 26 -20 25
18 Sunderland 26 -16 24
19 Cardiff 27 -29 22
20 Fulham 27 -32 21

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad