Watahiniwa wa kike wamefanya vizuri kwa kuchukua nafasi saba kati ya 10 za juu, huku Shule ya Marian Girls ya Pwani ikiongoza kwa kuwa na wanafunzi wanne. |
Mwanafunzi
aliyeongoza ni Robina Nicholaus wa Shule ya Marian Girls, akifuatiwa na Magrath
Kakoko wa St Francis (Mbeya) wakati wa tatu ni Joyceline Marealle kutoka Shule
ya Canossa (Dar es Salaam).
Wengine ni Safarina
Mariki na Abby Sembuche wa Marian Girls, wakati wavulana pekee kwenye wanafunzi
10 bora ni Sunday Mrutu kutoka Anne Marie (Dar es Salaam) na Nelson Rugola
Anthony na Emmanuel Mihuba Gregory wa Kaizirege (Kagera).
Wanaofuata ni Janeth
Urassa kutoka Marian Girls (Pwani) na Angle Ngulumbi wa St Francis (Mbeya).
Wasichana
10 bora.
Wasichana waliofanya
vizur kwenye mtihani huo wameongozwa na Robina Nicholaus (Marian Girls),
Magrath Kakoko (St Francis), Joyceline Leonard Marealle (Canossa), Safarina W
Mariki, Abby T Sembuche na Janeth Urassa (Marian Girls).
Wengine ni Angle
Ngulumbi (St Francis), Getrude James Mande wa Precious Blood (Arusha), Violet
Mwasenga wa St Francis na Catherine Swai kutoka Marian Girls.
Wavulana
10 Bora.
Wavulana waliofanya
Vizuri ni Sunday Mrutu wa Anne Marie, Nelson Rugola Anthony na Emanuel Mihuba
Gregory wote kutoka Kaizirege, Razack Hassan wa St Matthew’s (Pwani) na Hamis
Msangi kutoka Eangles (Pwani).
Wengine ni Joshua
Zumba wa Uwata (Mbeya), Brian Laurent na Mohamed Ally wa Marian Boys (Pwani),
Shahzill Msuya wa St Amedeus (Kilimanjaro) na Shabani Hamisi Maatu wa Mivumon
Islamic Seminary (Dar es Salaam).
Shule
za serikali hoi.
Matokeo yanaonyesha
kuwa shule kumi za kwanza ni za binafsi tu na shule za Serikali zimeanguka
vibaya.
Shule
bora
:-Ni St. Francis Girls ya Mbeya, Marian Boys ya Pwani, Feza Girls ya Dar es Salaam,
Precious Blood ya Arusha, Canossa ya Dar es Salaam, Marian Girls ya Pwani,
Anwarite Girls ya Kilimanjaro, Abbey ya Mtwara, Rosmin ya Tanga na Don Bosco Seminary
ya Iringa.
Katika shule zenye
watahiniwa chini ya 40 shule iliyoongoza ni Kaizirege ya Kagera, Alliance Girls
ya Mwanza, Thomas More Machrina ya Dar es Salaam, Mwanza Alliance ya Mwanza na
Queen of Apostles Ushirombo Seminary ya Geita.
Nyingine ni St Joseph Kilocha Seminary ya Njombe, Bethelsabs Girls ya Iringa, St Mary Junior Seminary ya Pwani, Maua Seminary ya Kilimanjaro na Hellen’s ya Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment