Mchezaji wa
Rhino akiuchota mpira kutoka kwa mchezaji wa Kagera Sugar.
|
Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara, jana Februari 22,2014 kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wameitandika Ruvu Shooting Bao 7-0 na kukamata uongozi wa Ligi.
Yanga SC , wakimchezesha kwa mara ya kwanza Straika kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, walikuwa mbele kwa Bao 4-0 hadi Mapumziko huku Bao la Kwanza likifungwa na Didier Kavumbagu ndani ya Sekunde 40 tu tangu Mechi ianze.
Yanga SC walipata Bao la Pili katika Dakika ya pili tu Mfungaji akiwa Simon Msuva na Emmanuel Okwi kufungua akaunti yake ya Magoli ya Ligi kwa Yanga katika Dakika ya 27 alipopiga Bao la 3.
Mrisho Ngassa alifunga Bao la 4 Dakika ya 30 na hadi Haftaimu Yanga walikuwa mbele 4-0.
Kipindi cha Pili Yanga SC waliongeza Bao 3 kupitia Kavumbagu, Msuva na Kiiza.
Huko Mkwakwani Jijini Tanga, Coastal Union waliichapa Mbeya City Bao 2-0 kwa Bao za Chipukizi Mohamed Miraji aliefunga katika Dakika ya 80 na 92.
Ligi Kuu
Vodacom 2013/2014:-RATIBA/MATOKEO.
Jumamosi
Februari 22,2014.
Ruvu Shooting 0
Yanga 7
Kagera Sugar 1
Rhino Rangers 0
Mtibwa Sugar 2
Ashanti United 1
Coastal Union 2
Mbeya City 0
Oljoro JKT 1
Mgambo JKT 2
Ligi Kuu Vodacom 2013/2014:-RATIBA.
Simba v JKT Ruvu
Azam FC v Tanzania Prisons
Jumatano Februari 26,2014.
Azam FC v Ashanti United
MSIMAMO.
NA | TIMU | P | W | D | L | GD | PTS |
1 | Yanga SC | 17 | 11 | 5 | 1 | 29 | 38 |
2 | Azam FC | 16 | 10 | 6 | 0 | 19 | 36 |
3 | Mbeya City | 19 | 9 | 8 | 2 | 8 | 35 |
4 | Simba SC | 18 | 8 | 8 | 2 | 17 | 32 |
5 | Kagera Sugar | 19 | 6 | 8 | 5 | 1 | 26 |
6 | Coastal Union | 19 | 5 | 10 | 4 | 5 | 25 |
7 | Mtibwa Sugar | 19 | 6 | 7 | 6 | 0 | 25 |
8 | Ruvu Shooting | 18 | 6 | 7 | 5 | -4 | 25 |
9 | JKT Ruvu | 18 | 6 | 1 | 11 | -14 | 19 |
10 | Mgambo JKT | 19 | 4 | 5 | 10 | -17 | 17 |
11 | Prisons FC | 16 | 3 | 7 | 6 | -3 | 16 |
12 | Ashanti United | 18 | 3 | 5 | 10 | -15 | 14 |
13 | JKT Oljoro | 19 | 2 | 8 | 9 | -15 | 14 |
14 | Rhino Rangers | 19 | 2 | 7 | 10 | -11 | 13 |
No comments:
Post a Comment