|
Wananchi wa Kijiji cha Mangae wakiwa wamefunga Barabara wakiwa wamishika
mawe na Silaha za Jadi wakikataa
kabisa kufungua barabara hiyo wakitaka Mkuu wa Mkoa kuja Kuoanana Nao.
|
Mabomu ya machozi yametumika kuwatawanya wakulima wa eneo la Melela,
Mvomero mkoani Morogoro waliokuwa wamefunga barabara ya Iringa - Morogoro
wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aende kusuluhisha mgogoro
uliopo baina yao na wafugaji. Wakulima wa kijiji cha Mangae wilaya Mvomero
wamefunga barbara kuu ya Morogoro Wakulima hao ambao wanalima katika Mashamba
yaliopo eneo la Mkangazi.
baada ya wananchi kuvamiwa na kupigwa wakulima hao walikusanyikajana
usiku na kufikia maamuziWakulima hao wanadai kuwa wenzao watano jana wamevamiwa
na wafugaji wa kabila la Wamasai na kuwajeruhi vibaya kwa vitu vyenye ncha kali
na kupelekea kulazwa katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alifika eneo hilo ambapo
wananchi hao walikuwa wamechoma matairi na kusababisha mgongamano mkubwa wa magari
yaendayo Iringa na yale yaelekeayo Moro lakini wakulima hao walikataa
kumsikiliza wakimtaka mkuu wa mkoa.
Baada ya vurugu kuwa kubwa, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile aliwaaamuru vijana wake wawatawanye
wakulima hao ambao waligoma na kuanza kuwapiga kwa mawe kitendo kilichopelekea
polisi kupiga mabomu ya machozi na kufanikiwa kuwatawanya.
Wananchi takribani 20
wamekamatwa na polisi katika vurugu hizo.Kwa sasa hali kidogo imetulia na
magari yameanza kupita eneo hilo.
|
Askari wa
Jeshi la Polisi Wakiwa Onyo wakulima wa Kijiji Hicho Kabla ya Kuanza Kutumia
Mabomu ya Kutoa Machozi kwa Lengo la Kuwatanya.
|





No comments:
Post a Comment