Arsenal
imepoteza nafasi ya kurejea tena kileleni mwa ligi kuu ya Premier, baada ya
kutoka sare ya kutofungana bao lolote na Manchester United katika uwanja wao wa
nyumbani wa Emirates.
|
Olivier
Giroud naye alipoteza nafasi nzuri zaidi ya Arsenal ya kufunga Man United.
|
Aliyekuwa
mchezaji wa Arsenal Robin Van Persie, nusura aifunge klabu yake ya zamani
lakini juhudi zake zilizimwa na Wojciech Szczesny.
|
Vijana hao
wa Arsene Wenger, walikuwa wakijaribu kufuta aibu waliopata wiki iliyopita
wakati walipofungwa magoli 5-1 na Liverpoool nayo Manchester United, kwa upande
wake ilikuwa ikijinasua baada ya kutoka sare ya kufungana magoli mawili kwa
mawili na Fulham mwishoni mwa juma lililopita.
Licha ya
kuwa mechi hiyo ilikosa ladha ya hadhi ya timu mbili kuu zinapocheza, pande
hizo mbili zilipoteza nafasi nyingi za kufunga.
Arsenal
inabaki nafasi ya pili kwa kutimiza pointi 56 baada ya kucheza mechi 26 sawa na
Chelsea yenye pointi 57 kileleni. United yenyewe imejiongezea moja na kufikisha
42 baada ya kucheza mechi 26 na inaendelea kukaa nafasi ya saba.
Steve
Gerrard aliifungia Liverpool, kupitia mkwaju wa penalti dakika za mwisho mwisho
na kuisaidia klabu yake kuilaza Fulham 3-2.
Bao la
kujifunga la Kolo Toure, liliipa Fulham uongozi kabla ya Daniel Sturridge
kusawazisha.
|
Lakini kadri
mechi hiyo ilipoendelea Fulham, walionyesha mchezo mzuri na kuongeza bao la
pili kupitia mchezaji Kieran Richardson baada ya mlinda lango wa Liverpool
Martin Skrtel kufanya masihara, kwenye eneo la hatari.
Uongozi wa
Fulham hata hivyo haukudumu kwa muda, pale Phillippe Coutinho kuisawazishia
Liverpool.
Timu hizo
mbili zilionekana kugawana alama moja kila mmoja lakini Liverpool, ilibahatika
pale Sascha Riether alipomfanyia madhambi Daniel Sturridge katika muda wa
ziada.
Nahodha wa
Liverpool Steve Gerrard, bila ya kusita alitinga bao la tatu na kuifanya
Liverpool kuwa alama nne tu nyuma ya vinara wa ligi hiyo kwa sasa Chelsea.
Position | Team | Played | Goal Difference | Points |
---|---|---|---|---|
1 | Chelsea | 26 | 27 | 57 |
2 | Arsenal | 26 | 22 | 56 |
3 | Man City | 25 | 41 | 54 |
4 | Liverpool | 26 | 34 | 53 |
5 | Tottenham | 26 | 4 | 50 |
6 | Everton | 25 | 11 | 45 |
7 | Man Utd | 26 | 10 | 42 |
8 | Southampton | 26 | 8 | 39 |
9 | Newcastle | 26 | -6 | 37 |
10 | Swansea | 26 | -3 | 28 |
11 | West Ham | 26 | -5 | 28 |
12 | Aston Villa | 26 | -9 | 28 |
13 | Hull | 26 | -6 | 27 |
14 | Stoke | 26 | -14 | 27 |
15 | Crystal Palace | 25 | -16 | 26 |
16 | Norwich | 26 | -20 | 25 |
17 | West Brom | 26 | -8 | 24 |
18 | Sunderland | 25 | -13 | 24 |
19 | Cardiff | 26 | -25 | 22 |
20 | Fulham | 26 | -32 | 20 |
Ushindi huo
ulikuwa wa tano wa Liverpool, mwaka huu na hii inamaanisha kuwa vijana hao wa
Brendan Roggers wangali na nafasi ya kutwaa kombe hilo la ligi kuu mwaka huu na
pia kudumisha rekodi ya kutoshindwa mechi yoyote mwaka huu.
|
Wakati huo
huo, hali mbaya ya anga ilisababisha mechi mbili za ligi kuu ya Uingereza kuhairishwa
jana usiku.
Mechi kati
ya Manchester City na Everton ilihairishwa kutokana na upepo mkali ili hali
mjini Everton, Polisi waliwashauri masimamizi wa klabu hiyo kuhairisha mechi
yao na Cyrstal Palace kwa sababu jengo moja lililokuwa karibu na uwanja huo
uliporomoka.
No comments:
Post a Comment