Tazama Picha CHADEMA na kura za maoni Jimbo la kalenga mwanasheria SINKALA MWENDA akiwashinda vibaya Wanachama wenzake 13. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 13, 2014

Tazama Picha CHADEMA na kura za maoni Jimbo la kalenga mwanasheria SINKALA MWENDA akiwashinda vibaya Wanachama wenzake 13.


Wajumbe  wa  mkutano  wa  kura  za  maoni  jimbo la  kalenga  kupitia  chama  cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wakifuatilia  matokeo ya  uchaguzi Jana februari 12,2014 katika  ukumbi  wa St Dominic mjini  Iringa.

Mshindi wa  kura za maoni jimbo la  kalenga mwanasheria  SINKALA  MWENDA  akipongezwa ….MWANASHERIA    Sinkala Mwenda  amefanikiwa  kuwashinda  vibaya wanachama wenzake 13  waliojitokeza  kuomba kuteuliwa  kuwa  wagombea  ubunge  jimbo la Kalenga  kupitia  chama  cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) huku kada aliyekimbia CCM kwa  kushindwa katika kura za maoni mwaka 2010  Zubery Mwachura  akijikuta  akiangukia  pua ndani ya Chadema kwa kukosa  kura  hata  moja katika uchaguzi  huo.
Kada  aliyeshika  nafasi ya  pili ktika mchakato  huo GRACE TENDEGA kushoto  akiwa na  wagombea  wenzake.
Kada  muuza magazeti Aidani Pungili kushoto akiwa na  wagombea  wenzake.
Msimamizi  mkuu wa  uchaguzi  huo Bw Benison Kigaila  akitoa  maelekezo ya  chama.
Mwenda  ametangazwa  mshindi  wa  kura za maoni  katika  uchaguzi  uliofanyika  leo  toka majira ya saa 4 asubuhi na kumalizika majira ya saa 4 usiku  katika  ukumbi  wa St Dominic mjini  Iringa  .

Uchaguzi  huo  uliosimamiwa na mjumbe  wa kamati  kuu ya Chadema Taifa Chiku  Abwao  na Benison  Kigaila  wajumbe  wa mkutano  wa Halmashauri  kuu ya  Chadema jimbo la kalenga   waliumiza  vichwa  vyao  kuwasikiliza wagombea  wote  13 kabla ya  kuwachuja na  kumchangua mwanasheria  Mwenda  kwa  kura 132  dhidi ya kura 122 alizopata mpinzani  wake wa karibu Grace Tendega ambae  pia  alikuwa akipewa nafasi  kubwa ya  kushinda  kutokana na kuwa na historia ya kugombea kupitia chama cha  Jahazi Asilia na kutoa ushindani mkali kwa CCM kabla ya  kuhamia Chadema.

Mbali  ya  wapinzani hao  wakubwa kuvutana vikali bado   kada  muuza magazeti  maarufu mjini  Iringa Aidan  Pungili  ambae  pia  alikuwa akipewa nafasi  ya  kufanya  vizuri  katika uchaguzi  huo  aliambulia kura 2 pekee huku mwenzake Daniel Luvanga akipata  kura  moja  ya  kufutia machozi .

Wagombea  wengine ambao  wameonyesha  kufanya vema kiasi  baada ya  kujiunga na Chadema  wakitokea  CCM ni pamoja na Dr Evaristo Mtitu  aliyepata  kura 32,Ancent Sambala ambae  amepata  kuwania ubunge katika kura za maoni CCM kwa zaidi ya mara 2 katika  jimbo la kalenga kabla ya kuhamia Chadema pia  aliambulia nafasi  ya  tano  kwa  kupata  kura 22 tofauti na nafasi  saba aliyochukua mwaka 2005 akiwa ndani ya CCM kwa kupata  kura chini ya 8.

Pia  mgombea Akbar Sanga  katika uchaguzi huo  alipata kura (21),Rehema Makoga (4), Henry Kavina(9), Mussa Mdede(48), Mchungaji Samweli  Nyakunga(2) na mwalimu Vitus Lawa akipata kura (14).

Msimamizi  mkuu wa  uchaguzi  huo mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila aliwataka wajumbe  wa  mkutano  huo kutoshangilia zaidi juu ya matokeo hayo kwani  kushinda  katika  kinyang'anyiro ni mwanzo tu wa  safari  ya  kumpata mteule wa Chadema atakayekabidhiwa bendera  ya  Chadema  kuvaana na CCM katika uchaguzi huo mdogo.

Alisema mgombea sahihi ambae  watapaswa kumshangilia na kumtangaza kwa  wananchi  wa jimbo la Kalenga ni  yulev ambae atapitishwa na vikao  vya juu vya  Chama  hicho Taifa tarehe 14 mwezi huu.

Hata  hivyo  aliwataka  wagombea  wote 13  walioomba kuwania nafasi  hiyo kabla ya kupatikana mshindi  huo Mwenda  kuanza safari mapema kesho Alhamis asubuhi ya kwenda  jijini Dar es salaam  kwa ajili ya  kwenda kujieleza mbele ya kamati  kuu ya  Chadema kabla ya  kumteua mgombea  wa jimbo  hilo la kalenga.

"Baada ya  matokeo haya  ndugu zangu wajumbe  nawaombeni  makatibu  kata wote  wa jimbo la Kalenga  kubaki hapa ndani na wajumbe kuanza  safari ya  kurudi majumbani  leo  hata  hatutaruhusu wagombea  ama mshindi  kuongea  chochote  .....kwani  wote  watakwenda  kuongea mbele ya kamati  kuu ila kuanzia kesho  Chadema itaendelea na mikutano  yake  jimbo la kalenga ya  kukitambulisha chama zaidi  kwa wananchi na sio kumnadi mgombea kwani bado mgombea  wetu  hajapatikana kampeni zenyewe  zitaanza baada ya  mgombea  wetu atakayeteuliwa kuchukua  na kurejesha  fomu ya tume"

Kigaila  aliwataka  viongozi hao wa Chadema jimbo la kalenga  kuanza kukijenga  zaidi  chama  hicho na kuwa mara  baada ya  kampeni kuanza  wana Chadema wilaya  zote za mkoa  wa Iringa  wataingia kazini  katika  jimbo  hilo.

VITUKO  VYA  WAGOMBEA

Mmoja kati ya  wagombea  walioomba ashindwa kutokea  ukumbini atuma mpambe  kumsomea  maelezo  yake  huku akieleza  kuwa iwapo atapitishwa  kuwa mgombea tayari  ametenga  kiasi cha Tsh milioni 9 kwa ajili ya kampeni zake kitendo cha kutofika ukumbini hapo  kilionyesha kuwakwaza  wajumbe  kuwa  hawana shida na pesa  zake hivyo kumnyima nafasi hiyo.

Huku  kituko namba  mbili kutoka kwa  wagombea  hao ni baada ya mmoja wapo kudanganya  kiwango  chake  cha elimu na kuongopa chuo alichopata  elimu  yake na kushindwa kutamka vema kiwango cha elimu alicho nacho hivyo wajumbe kushindwa kuamini maelezo yake na kumnyima pia kura.

Kituko  kikubwa cha  tatu ni pale  mmoja kati ya  wagombea kutumia CV yake ya  kufungwa  jela mara kwa mara kama mtaji wa kuombea  kura  huku  wajumbe  hao wakishindwa kujua umaarufu  wake  wa kufungwa na maendeleo ya wana Kalenga vina mahusiano gani hivyo kumpiga  chini pia.


Habari Na:- Francis godwin blog
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad