Lori la
mafuta baada ya kuteketea kwa moto kijiji cha Fulwe, Eneo la Mikese mkoani
Morogoro leo Februari 23,2014.
|
Lori la
mafuta na semitrela vikiteketea kwa moto baada ya ajali.
|
Semitrela
lenye namba za usajili T 499 AUD baada ya ajali hiyo.
|
Wananchi
wakibeba mwili wa dereva wa lori ulioteketea kwenye moto.
|
Askari wa
Kikosi cha Zimamoto wakijaribu kutuliza moto huo.
|
Zoezi la
kuzima moto na kusafisha barabara likiendelea.
|
Gari la
Kikosi cha Zimamoto likiwa eneo la ajali.
|
Kijiji cha
Fulwe ilipotokea ajali hiyo.
|
AJALI hii
imetokea leo februari 23,2014, katika kijiji cha Fulwe, kata ya Mikese mkoani Morogoro ambapo
malori mawili yamegongana na kuteketea kwa moto.
Katika ajali
hiyo, dereva wa lori moja lililokuwa na shehena ya mafuta amepoteza maisha
wakati dereva wa lori lingine aina ya semitrela akijeruhiwa pamoja na tingo
wake na kukimbizwa hospitali.
Mmoja wa
mashuhuda wa ajali hiyo amedai kuwa dereva aliyepoteza maisha alishindwa
kujiokoa baada ya ajali kutokea kwa kubanwa hali iliyopelekea kuungua vibaya
kwa moto.
"Lori
hili la mafuta lilikuwa likitoka Dar na kushuka mteremeko huu kwa kasi huku
semitrela likijaribu kulipita lori lingine eneo hili hivyo kugongana uso kwa na
lori la mafuta.
Baada ya
kugongana, mafuta yaliokuwa kwenye tenki yalimwagika hali iliyosababisha malori
yote kuteketea kwa moto. " Alisema shuhuda huyo mkazi wa kijiji cha Fulwe,
Bw Issa Athuman.
(PICHA ZOTE
NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL)
No comments:
Post a Comment