Matokeo hayo ya leo Februari 23,2014,yanamaanisha, Yanga SC iliyoshinda 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting jana Februari 22,2014 Uwanja wa Taifa, inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 38, Azam ya pili 37 na Mbeya City ya tatu 35 na Simba SC ya nne 32.
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hadi mapumziko JKT Ruvu walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyotiwa kimiani na Hussein Bunu dakika ya 14 na Emmanuel Swita dakika ya 44 kwa penalti, baada ya Henry Joseph kumuangusha Amos Mgisa kwenye eneo la hatari.
Hata hivyo, penalti hiyo ilionekana kuwa ya utata, kwani mguu wa Henry ulionekana kwenda kuuondosha mpira miguuni mwa Mgisa bila kumgusa mchezaji huyo.
Kipindi cha pili, JKT Ruvu ilionekana kurudi na moto wake tena na kufanikiwa kupata bao la tatu mapema dakika ya 52, mfungaji Emmanuel Swita tena kwa shuti kali baada ya pasi ya Amosi Mgisa.
Simba SC ilizinduka baada ya bao hilo na kupambana hadi kupata mabao mawili yaliyofungwa na Mrundi Amisi Tambwe dakika za 64 kwa penalti baada ya Amri Kiemba kuangushwa kwenye eneo la hatari na dakika ya 84, akiunganisha krosi ya Kiemba.
Huko uwanja Azam
Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Wenyeji Azam FC
waliikosa nafasi ya kutwaa uongozi wa Ligi toka kwa Yanga baada kutoka Sare ya
2-2 na Tanzania Prisons.
Hadi
Mapumziko Bao zilikuwa 0-0.
Prisons ndio
waliofunga Bao la Kwanza katika Dakika ya 47 kwa Frikiki ya Omega Seme na Azam
kusawazisha chapchap katika Dakika ya 49 kwa Bao la Aggrey Morris na kupiga Bao
la Pili Dakika moja baadae kwa Bao la Kipre Tcheche.
Haikuchukua
muda kwa Kipre Tcheche kupewa Kadi ya Njano ya Pili na hivyo kutolewa nje kwa
Kadi Nyekundu na hii iliwapa mwanya Prisons ambao hatimae kwenye Dakika ya 80
walisawazisha kwa Bao la Mpalile.
Jumatano Februari 26,2014.
Azam FC v Ashanti United
MSIMAMO VPL 2013/2014.
NA | TIMU | P | W | D | L | GD | PTS |
1 | Yanga SC | 17 | 11 | 5 | 1 | 29 | 38 |
2 | Azam FC | 17 | 10 | 7 | 0 | 19 | 37 |
3 | Mbeya City | 19 | 9 | 8 | 2 | 8 | 35 |
4 | Simba SC | 19 | 8 | 8 | 3 | 16 | 32 |
5 | Kagera Sugar | 19 | 6 | 8 | 5 | 1 | 26 |
6 | Coastal Union | 19 | 5 | 10 | 4 | 5 | 25 |
7 | Mtibwa Sugar | 19 | 6 | 7 | 6 | 0 | 25 |
8 | Ruvu Shooting | 18 | 6 | 7 | 5 | -4 | 25 |
9 | JKT Ruvu | 19 | 7 | 1 | 11 | -13 | 22 |
10 | Prisons FC | 17 | 3 | 8 | 6 | -3 | 17 |
11 | Mgambo JKT | 19 | 4 | 5 | 10 | -17 | 17 |
12 | Ashanti United | 18 | 3 | 5 | 10 | -15 | 14 |
13 | JKT Oljoro | 19 | 2 | 8 | 9 | -15 | 14 |
14 | Rhino Rangers | 19 | 2 | 7 | 10 | -11 | 13 |
No comments:
Post a Comment