Simba yatoka hoi huko Mkwakwani, Mbeya City yaichapa Mtibwa Sugar 2 -1 na kurejea nafasi ya 3 Ligi Kuu soka Vodacom Tanzania bara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, February 10, 2014

Simba yatoka hoi huko Mkwakwani, Mbeya City yaichapa Mtibwa Sugar 2 -1 na kurejea nafasi ya 3 Ligi Kuu soka Vodacom Tanzania bara.


Kikosi cha Timu ya Mgambo JKT ambapo ….Kwenye Mechi za VPL, Ligi Kuu Vodavom, huko Mkwakwani, Jijini Tanga, Simba SC wamefungwa Bao 1-0 na Mgambo JKT na kung’olewa kutoka Nafasi ya 3 na Mbeya City ambao wamewachapa Mtibwa Sugar Bao 2-1 huko Sokoine, Mbeya wakati Coastal Union wakipata ushindi adimu huko Tabora kwa kuitungua Rhino.
Kikosi cha timu ya Mbeya City ambao wamewachapa Mtibwa Sugar Bao 2-1 huko Sokoine, Mbeya katika mchezo wa Ligi kuu soka Vodacom Tanzania bara leo Feb 09,2014.
Bao ambalo limeua Simba SC huko Jijini Tanga lilifungwa katika Dakika ya 29 na Fully Maganga.

Kwa matokeo hayo, Simba SC inabaki na pointi zake 31 baada ya kucheza mechi 17, wakati Mgambo inatimiza pointi 12 na inaendelea kushika mkia.

Katika mchezo wa Mbeya City na Mtibwa Sugar,Mabao ya Mbeya City leo Feb 09,2014 yamefungwa na Peter Michael dakika ya pili na Hamad Kibopile dakika ya 67, wakati la Mtibwa limefungwa na Jamal Mnyate dakika ya 53.

Mbeya City sasa wanatimiza pointi 34 na kurejea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya Yanga SC pointi 35 na Azam FC 36.

Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora bao pekee la Haruna Moshi Shaaban ‘Boban’ dakika ya nane limeipa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Rhino Rangers.

Kagera Sugar wamelazimisha sare ya 1-1 ugenini Uwanja wa Sheikh Amri Abeid dhidi ya wenyeji JKT Oljoro. 

Bao la Kagera limefungwa na Themi Felix dakika ya saba na Oljoro wakasawazisha kupitia kwa Jacob Masawe dakika ya 82.

Mapema jana(Februari 08,2014) Tanzania Prisons iliifunga mabao 3-1 Ruvu Shooting, mabao yake yakitiwa kimiani na Michael Peter dakika ya 56, Jeremiah Juma dakika ya 85 na Laurian Mpalile dakika ya 89 ambaye alijifunga pia dakika ya 85 kuwapatia wapinzani wao bao la kufutia machozi.


RATIBA MECHI ZIJAZO LIGI KUU SOKA VODACOM TANZANIA BARA.

Jumatano Februari 12,2014.

JKT Ruvu v Ruvu Shooting

Jumamosi Februari 15,2014.

Rhino Rangers v Mgambo JKT
Ashanti United v Kagera Sugar
Mtibwa Sugar v Tanzania Prisons
JKT Oljoro v JKT Ruvu
Mbeya City v Simba
Ruvu Shooting v Coastal Union


NO
TEAMS
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Azam FC
16
10
6
0
29
10
19
36
2
Yanga
16
10
5
1
34
12
22
35
3
Mbeya City
17
9
7
1
24
14
10
34
4
Simba SC
17
8
7
2
33
15
18
31
5
Coastal Union
17
4
10
3
12
8
4
22
6
Mtibwa Sugar
17
5
7
5
21
21
0
22
7
Kagera Sugar
17
5
7
5
16
16
0
22
8
Ruvu Shootings
15
4
7
4
16
16
0
19
9
JKT Ruvu
15
6
0
9
13
19
-6
18
10
JKT Oljoro
17
2
7
8
13
18
-5
13
11
Ashanti United
16
3
4
9
14
28
-14
13
12
Mgambo JKT
17
3
4
10
8
26
-18
13
13
Rhino Rangers
17
2
6
9
11
21
-10
12
14
Tanzania Prisons
14
1
7
6
6
16
-10
10

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad