![]() |
|
Kiungo
mkabaji wa Ferroviario, de Beira akipiga tik tak dhidi ya mshambuliaji wa Azam
FC, Brian Umony leo(Februari 09,2014) Chamazi.
|
Timu ya Azam
FC imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0, leo (Feb 09,2014) dhidi ya Ferroviario
de Beira ya Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la
Shirikisho Afrika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaa.
Shukrani
kwake mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche aliyefunga bao
hilo pekee dakika ya 41 baada ya kutengewa pasi nzuri ya kichwa na Mganda Brian
Umony na kufumua shuti kali.
Mchezo
ulikuwa mkali dakika zote 90 na mashambulizi yalikuwa ya pande zote mbili.
Matokeo hayo
yanamaanisha Azam FC itakuwa na kazi ngumu katika mchezo wa marudiano wiki mbili
zijazo nchini Msumbiji, wakitakiwa kulazimisha sare ili kusonga mbele.








No comments:
Post a Comment