THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL
COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S
OFFICE,
THE STATE
HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU
UTEUZI WA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA
UTANGULIZI
1.
Uteuzi
wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,
Sura, 83 (The Constitutional Review Act,
Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo
na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge
la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha
umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika.
2.
Sheria
hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:-
(i)
Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(ii)
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
(iii)
Wajumbe 201
kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.
3.
Makundi hayo ni
kama ifuatavyo:-
(i)
Taasisi
zisizokuwa za Kiserikali (20)
(ii)
Taasisi
za Kidini (20)
(iii)
Vyama
vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42);
(iv)
Taasisi
za Elimu (20);
(v)
Watu
wenye Ulemavu (20);
(vi)
Vyama
vya Wafanyakazi (19);
(vii)
Vyama
vinavyowakilisha Wafugaji (10);
(viii)
Vyama
vinavyowakilisha wavuvi (10);
(ix)
Vyama
vya Wakulima (20); na
(x)
Vikundi
vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).
4.
Mchakato
wa uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13
Desemba, 2013. Tangazo hilo lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza
ili kuyaalika makundi yaliyotajwa kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina
kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum la Katiba. Aidha, Tangazo hilo la
mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini.
Pamoja na mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi
na Makundi kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe
02/01/2014.
5.
Mapendekezo
hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar,
mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar.
6.
Kufuatia
mwaliko huo, taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178 kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao. Mapendekezo hayo
yalijumuisha majina 2,762 kwa upande
wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar mapendekezo hayo yalihusisha watu 874.
Hivyo
basi, taasisi na makundi mbalimbali yalipendekeza jumla ya majina 3,636. Lakini, na kinyume na Sheria,
watu 118 walijipendekeza wenyewe na
kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754.
7.
Mchanganuo
wa idadi ya watu walipendekezwa katika makundi mbalimbali ni kama ifuatavyo:
|
Na.
|
Kundi/Taasisi
|
Taasisi
zilizoleta mapendekezo
|
Idadi ya
Watu Waliopendekezwa
|
Idadi ya
Wajumbe Wanaotakiwa
|
Idadi ya
Walioteuliwa
|
|||
|
Tanzania
Bara
|
Zanzibar
|
Tanzania
Bara
|
Zanzibar
|
Tanzania
Bara
|
Zanzibar
|
|||
|
1.
|
Taasisi zisizokuwa za Kiserikali
|
246
|
98
|
1,203
|
444
|
20
|
13
|
7
|
|
2.
|
Taasisi za Kidini
|
55
|
17
|
344
|
85
|
20
|
13
|
7
|
|
3.
|
Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa
Kudumu
|
21
|
14
|
129
|
69
|
42
|
28
|
14
|
|
4.
|
Taasisi za Elimu
|
9
|
9
|
84
|
46
|
20
|
13
|
7
|
|
5.
|
Makundi ya Walemavu
|
24
|
6
|
97
|
43
|
20
|
13
|
7
|
|
6.
|
Vyama vya Wafanyakazi
|
20
|
1
|
89
|
13
|
19
|
13
|
6
|
|
7.
|
Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji
|
8
|
1
|
43
|
4
|
10
|
7
|
3
|
|
8.
|
Vyama vinavyowakilisha Wavuvi
|
7
|
3
|
45
|
12
|
10
|
7
|
3
|
|
9.
|
Vyama vya Wakulima
|
22
|
8
|
115
|
44
|
20
|
13
|
7
|
|
10.
|
Makundi yenye Malengo Yanayofanana
|
142
|
21
|
613
|
114
|
20
|
14
|
6
|
|
Mapendekezo Binafsi
|
-
|
-
|
118
|
-
|
||||
|
Jumla
|
672
|
178
|
2,880
|
874
|
201
|
134
|
67
|
|
|
Jumla Kuu
|
850
|
3,754
|
||||||
8.
Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba imeweka masharti ya kuzingatiwa katika uteuzi wa
wajumbe 201 wa Bunge la Maalum la Katiba.
Masharti
hayo ni pamoja na wajumbe wasiopungua theluthi moja wanatakiwa kutoka Zanzibar
na theluthi mbili kutoka Tanzania Bara.
Kwa
sababu hiyo, katika wajumbe 201, wajumbe 67 watatoka Zanzibar na wajumbe
134 watatoka Tanzania Bara.
Aidha,
mgawanyo wa wajumbe wanawake na wanaume unatakiwa uwe nusu kwa nusu. Pamoja na
hayo, wajumbe hao wawakilishe sura ya wananchi wa Tanzania kwa ufuasi wa vyama
vya siasa, dini, umri, na maeneo wanayotoka.
Katika
mazingira haya, zoezi la kupata wajumbe 201 halikuwa rahisi hata kidogo.
Mwitikio wa makundi ulikuwa mkubwa sana ikilinganishwa na nafasi zilizopo.
9.
Kama
nilivyoeleza hapo awali, mapendekezo kutoka Tanzania Bara yalikuwa 2,880 wakati
nafasi za wajumbe ni 134. Kwa upande wa Zanzibar, majina yaliyopendekezwa
yalikuwa 874 ikilinganishwa na idadi ya wajumbe 67 wanaotakiwa kuteuliwa. Kwa
nyongeza ya maelezo kuhusu uwingi wa mapendekezo, ni kwamba ukichukua taasisi
zisizo za kiserikali kwa upande wa Tanzania Bara walipendekezwa watu
1,203, wakati nafasi zilizokuwa zinatakiwa kujazwa ni 13 tu. Kwa upande
Zanzibar, taasisi zisizokuwa za kiserikali zilikuwa zimependekeza majina 444
ikilinganishwa na nafasi 7 tu zilizokuwa zinatakiwa kujazwa kutokana na taasisi
hizi.
WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA
10.
Rais
wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakishirikiana na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Zanzibar wamekamilisha uteuzi wa wajumbe 201.
Kabla ya kutaja orodha ya wajumbe walioteuliwa, napenda kufafanua mambo
yafuatayo:-
(a)
Uteuzi
umezingatia ushiriki wa watu wa rika zote, yaani vijana, watu wazima na wazee.
Kwa ajili hiyo, wajumbe vijana yaani wenye umri wa kati miaka 22-35, ni wajumbe
35. Wajumbe wenye umri wa kati, yaani miaka 36-64, ni 145; na wajumbe wazee,
yaani wenye umri wa miaka 65 na kuendelea ni 21.
(b)
Sheria
inataka kuwepo na uwiano sawa kwa ajumbe wanawake na wanaume. Jambo hili
limezingatiwa ipasavyo, na katika orodha hii wajumbe wanawake ni 100 na wanaume
101. Kwa vile, haiwezekani kuwa na nusu mtu, ndiyo maana idadi ya wajumbe
wanaume ni 101.
(c)
Uwakilishi
wa vyama vya siasa ambao unahitaji kila chama chenye usajili wa kudumu kiwe na
wajumbe wawili umezingatiwa. Kwa kuwa kuna vyama vya siasa vyenye usajili
wa kudumu 21, jumla ya wajumbe 42 wamechaguliwa kwa maana ya kuwa wajumbe
wawili wameteuliwa kutoka katika kila chama.
Baada
ya maelezo hayo ya utangulizi, ifuatayo ndiyo orodha ya wajumbe 201 wa Bunge
Maalum la Katiba waliobahatika kuteuliwa:
TAASISI ZISIZOKUWA ZA KISERIKALI- (WAJUMBE 20) |
|
TANZANIA BARA (13) |
|
|
1.
Magdalena Rwebangira
|
2.
Kingunge Ngombale Mwiru
|
|
3.
Asha
D. Mtwangi
|
4.
Maria Sarungi Tsehai
|
|
5.
Paul
Kimiti
|
6.
Valerie
N. Msoka
|
|
7.
Fortunate
Moses Kabeja
|
8.
Sixtus
Raphael Mapunda
|
|
9.
Elizabeth
Maro Minde
|
10.
Happiness
Samson Sengi
|
|
11. Evod Herman
Mmanda
|
12.
Godfrey
Simbeye
|
|
13. Mary Paul Daffa
|
|
|
TANZANIA ZANZIBAR (7)
|
|
|
1.
Idrissa
Kitwana Mustafa
|
2.
Siti
Abbas Ali
|
|
3.
Abdalla
Abass Omar
|
4.
Salama
Aboud Talib
|
|
5.
Juma
Bakari Alawi
|
6.
Salma
Hamoud Said
|
|
7.
Adila
Hilali Vuai
|
|
|
TAASISI ZA KIDINI- (WAJUMBE 20)
|
|
|
TANZANIA BARA (13)
|
|
|
1.
Tamrina
Manzi
|
2.
Olive
Damian Luwena
|
|
3.
Shamim
Khan
|
4.
Mchg.
Ernest Kadiva
|
|
5.
Sheikh
Hamid Masoud Jongo
|
6.
Askofu
Mkuu (Mstaafu) Donald Leo Mtetemela
|
|
7.
Magdalena
Songora
|
8.
Hamisi
Ally Togwa
|
|
9.
Askofu
Amos J. Muhagachi
|
10.
Easter
Msambazi
|
|
11.
Mussa
Yusuf Kundecha
|
12.
Respa
Adam Miguma
|
|
13.
Prof.
Costa Ricky Mahalu
|
|
|
TANZANIA ZANZIBAR (7)
|
|
|
1.
Sheikh
Thabit Nouman Jongo
|
2.
Suzana
Peter Kunambi
|
|
3.
Sheikh
Nassoro Mohammed Ibrahimu
|
4.
Fatma
Mohammed Hassan
|
|
5.
Louis
Majaliwa
|
6.
Yasmin
Yusufali E. H alloo
|
|
7.
Thuwein
Issa Thuwein
|
|
|
|
|
VYAMA VYOTE VYA SIASA
VYENYE USAJILI WA KUDUMU – (WAJUMBE
42)
|
|
|
TANZANIA BARA (28)
|
|
|
1.
Hashim
Rungwe Spunda
|
2.
Thomas
Magnus Mgoli
|
|
3.
Rashid
Hashim Mtuta
|
4.
Shamsa
Mwangunga
|
|
5.
Yusuf S. Manyanga
|
6.
Christopher
Mtikila
|
|
7.
Bertha
Ng’angompata
|
8.
Suzan
Marwa
|
|
9.
Dominick
Abraham Lyamchai
|
10.
Mbwana
Salum Kibanda
|
|
11.
Peter
Kuga Mziray
|
12.
Isaac
Manjoba Cheyo
|
|
13.
Dr.
Emmanuel John Makaidi
|
14.
Prof.
Ibrahim Haruna Lipumba
|
|
15.
Modesta
Kizito Ponera
|
16.
Prof.
Abdallah Safari
|
|
17.
Salumu
Seleman Ally
|
18.
James
Kabalo Mapalala
|
|
19.
Mary
Oswald Mpangala
|
20.
Mwaka
Lameck Mgimwa
|
|
21.
Nancy S. Mrikaria
|
22.
Nakazael
Lukio Tenga
|
|
23.
Fahmi
Nasoro Dovutwa
|
24.
Costantine Benjamini Akitanda
|
|
25.
Mary
Moses Daudi
|
26.
Magdalena
Likwina
|
|
27.
John
Dustan Lifa Chipaka
|
28.
Rashid
Mohamed Ligania Rai
|
|
TANZANIA ZANZIBAR (14)
|
|
|
1.
Ally
Omar Juma
|
2.
Vuai
Ali Vuai
|
|
3.
Mwanaidi
Othman Twahir
|
4.
Jamila
Abeid Saleh
|
|
5.
Mwanamrisho
Juma Ahmed
|
6.
Juma
Hamis Faki
|
|
7.
Tatu
Mabrouk Haji
|
8.
Fat
–Hiya Zahran Salum
|
|
9.
Hussein
Juma
|
10.
Zeudi
Mvano Abdullahi
|
|
11.
Juma
Ally Khatibu
|
12.
Haji
Ambar Khamis
|
|
13.
Khadija
Abdallah Ahmed
|
14.
Rashid
Yussuf Mchenga
|
|
TAASISI ZA ELIMU- (WAJUMBE 20)
|
|
|
TANZANIA BARA
|
|
|
1.
Dr.
Suzan Kolimba
|
2.
Prof.
Esther Daniel Mwaikambo
|
|
3.
Dr. Natujwa Mvungi
|
4.
Prof.
Romuald Haule
|
|
5.
Dr.
Domitila A.R. Bashemera
|
6.
Dr.
Jasmine Bendantunguka Tiisekwa
|
|
7.
Prof.
Bernadeta Kilian
|
8.
Teddy
Ladislaus Patrick
|
|
9.
Dr.
Francis Michael
|
10.
Prof.
Remmy J. Assey
|
|
11.
Dr.
Tulia Ackson
|
12.
Dr.
Ave Maria Emilius Semakafu
|
|
13.
Hamza
Mustafa Njozi
|
|
|
TANZANIA ZANZIBAR (7)
|
|
|
1.
Makame
Omar Makame
|
2.
Fatma
Hamid Saleh
|
|
3.
Dr.
Aley Soud Nassor
|
4.
Layla
Ali Salum
|
|
5.
Dkt.
Mwinyi Talib Haji
|
6.
Zeyana
Mohamed Haji
|
|
7.
Ali
Ahmed Uki
|
|
|
WATU WENYE ULEMAVU-(WAJUMBE 20)
|
|
|
TANZANIA BARA (13)
|
|
|
1.
Zuhura
Musa Lusonge
|
2.
Frederick
Msigala
|
|
3.
Amon
Anastaz Mpanju
|
4.
Bure
Zahran
|
|
5.
Edith
Aron Dosha
|
6.
Vincent
Venance Mzena
|
|
7.
Shida
Salum Mohamed
|
8.
Dr.
Henry Mwizengwa Nyamubi.
|
|
9.
Elias
Msiba Masamaki
|
10.
Faustina
Jonathan Urassa
|
|
11.
Doroth
Stephano Malelela
|
12.
John
Josephat Ndumbaro
|
|
13.
Ernest
Njama Kimaya
|
|
|
TANZANIA ZANZIBAR (7)
|
|
|
1.
Haidar
Hashim Madeweyya
|
2.
Alli
Omar Makame
|
|
3.
Adil
Mohammed Ali
|
4.
Mwandawa
Khamis Mohammed
|
|
5.
Salim
Abdalla Salim
|
6.
Salma
Haji Saadat
|
|
7.
Mwantatu
Mbarak Khamis
|
|
|
VYAMA VYA WAFANYAKAZI-(WAJUMBE 19)
|
|
|
TANZANIA BARA (13)
|
|
|
1.
Honorata
Chitanda
|
2.
Dr.
Angelika Semike
|
|
3.
Ezekiah
Tom Oluoch
|
4.
Adelgunda
Michael Mgaya
|
|
5.
Dotto
M. Biteko
|
6.
Mary
Gaspar Makondo
|
|
7.
Halfani
Shabani Muhogo
|
8.
Yusufu
Omari Singo
|
|
9.
Joyce
Mwasha
|
10.
Amina
Mweta
|
|
11.
Mbaraka
Hussein Igangula
|
12.
Aina
Shadrack Massawe
|
|
13.
Lucas
Charles Malunde
|
|
|
TANZANIA ZANZIBAR (6)
|
|
|
1.
Khamis
Mwinyi Mohamed
|
2. Jina Hassan
Silima
|
|
3.
Makame
Launi Makame
|
4. Asmahany Juma Ali
|
|
5.
Mwatoum
Khamis Othman
|
6. Rihi Haji Ali
|
|
VYAMA
VINAVYOWAKILISHAWAFUGAJI-(WAJUMBE 10)
|
|
|
TANZANIA BARA (7)
|
|
|
1.
William
Tate Olenasha
|
2.
Makeresia
Pawa
|
|
3.
Mabagda
Gesura Mwataghu
|
4.
Doreen
Maro
|
|
5.
Magret
Nyaga
|
6.
Hamis
Mnondwa
|
|
7.
Ester
Milimba Juma
|
|
|
TANZANIA ZANZIBAR (3)
|
|
|
1.
Said
Abdalla Bakari
|
2.
Mashavu
Yahya
|
|
3.
Zubeir
Sufiani Mkanga
|
|
|
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAVUVI
–(WAJUMBE 10)
|
|
|
TANZANIA BARA (7)
|
|
|
1.
Hawa
A. Mchafu
|
2.
Rebecca
Masato
|
|
3.
Thomas
Juma Minyaro
|
4.
Timtoza
Bagambise
|
|
5.
Tedy
Malulu
|
6.
Rebecca
Bugingo
|
|
7.
Omary
S. Husseni
|
|
|
TANZANIA ZANZIBAR (3)
|
|
|
1.
Waziri
Rajab
|
2.
Issa
Ameir Suleiman
|
|
3.
Mohamed
Abdallah Ahmed
|
|
|
VYAMA
VYAWAKULIMA-(WAJUMBE 20)
|
|
|
TANZANIA BARA
(13)
|
|
|
1.
Agatha Harun Senyagwa
|
2.
Veronica
Sophu
|
|
3.
Shaban
Suleman Muyombo
|
4.
Catherine
Gabriel Sisuti
|
|
5.
Hamisi
Hassani Dambaya
|
6.
Suzy
Samson Laizer
|
|
7.
Dr.
Maselle Zingura Maziku
|
8.
Abdallah
Mashausi
|
|
9.
Hadijah
Milawo Kondo
|
10.
Rehema
Madusa
|
|
11.
Reuben
R. Matango
|
12.
Happy
Suma
|
|
13.
Zainab
Bakari Dihenga
|
|
|
TANZANIA ZANZIBAR
(7)
|
|
|
1.
Saleh
Moh’d Saleh
|
2.
Biubwa
Yahya Othman
|
|
3.
Khamis
Mohammed Salum
|
4.
Khadija
Nassor Abdi
|
|
5.
Fatma
Haji Khamis
|
6.
Asha
Makungu Othman
|
|
7.
Asya
Filfil Thani
|
|
|
WATU WENYE
MALENGO YANAYOFANANA – (WAJUMBE 20)
|
|
|
TANZANIA BARA
(14)
|
|
|
1.
Dr.
Christina Mnzava
|
2.
Paulo
Christian Makonda
|
|
3.
Jesca
Msambatavangu
|
4.
Julius
Mtatiro
|
|
5.
Katherin
Saruni
|
6. Abdallah Majura
Bulembo
|
|
7.
Hemedi
Abdallah Panzi
|
8.
Dr.
Zainab Amir Gama
|
|
9.
Hassan
Mohamed Wakasuvi
|
10.
Paulynus
Raymond Mtendah
|
|
11.
Almasi
Athuman Maige
|
12.
Pamela
Simon Massay
|
|
13.
Kajubi
Diocres Mukajangwa
|
14.
Kadari
Singo
|
|
TANZANIA
ZANZIBAR (6)
|
|
|
1.
Yussuf
Omar Chunda
|
2.
Fatma
Mussa Juma
|
|
3.
Prof.
Abdul Sheriff
|
4.
Amina
Abdulkadir Ali
|
|
5.
Shaka
Hamdu Shaka
|
6.
Rehema
Said Shamte
|
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
7
Februari, 2014






No comments:
Post a Comment