Tayari wachezaji wengine wawili wa Yanga kutoka
Uganda, wameitwa kwenye timu yao ya soka ya taifa, The Cranes kwa ajili ya
mchezo dhidi ya Zambia mjini Ndola Machi 5, hao ni Emmanuel Okwi na Hamisi
Kiiza.
Ikumbukwe Yanga SC itacheza mechi ya marudiano na Al Ahly ya Misri mjini Cairo kati ya Machi 7 na 9 katika Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mchezo wa kwanza Dar es Salaam Machi 1, mwaka huu.
Kwa nyota hao nane kuitwa timu za taifa za Uganda na Tanzania dhahiri itaathiri maandalizi ya Yanga kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Ahly, kwani Okwi na Kiiza watalazimika kwenda Uganda mara tu baada ya mechi ya kwanza na mabingwa hao wa Afrika na kwa kuwa watacheza mechi Ndola Machi 5, maana yake wanaweza kuondoka huko Machi 6 wakati tayari mabingwa wa Bara wakiwa Cairo.
Na sita wa Stars wataingia kambini timu ya taifa baada ya mechi ya kwanza na Ahly na Machi 3 watasafiri kwenda Namibia na kucheza mechi Machi 5, hivyo kuondoka nchini humo siku inayofuata- maana yake nyota wote nane hawatapata fursa ya kushiriki mazoezi ya Yanga kujiandaa na mchezo wa marudiano na Ahly.
Hali itakuwa mbaya zaidi kwa Yanga iwapo na Rwanda itawaita Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima kwa ajili ya mechi za wiki ijayo za kalenda ya FIFA.
Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam) na Kelvin
Yondani (Yanga) wakati viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga),
David Luhende (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Jonas Mkude (Simba) na Mwinyi
Kazimoto (Markhiya Sports Club, Qatar).
Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance Mwanza),
Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Ramadhan Singano (Simba)
na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium
Lager itaingia kambini Machi 1 mwaka huu, kwenye hoteli ya Accommondia
inatarajiwa kuondoka Machi 3 mwaka huu kwenda Windhoek.
Wachezaji ambao timu zao zinacheza mechi za
mashindano ya kimataifa na ligi wikiendi hii wataripoti kambini mara baada ya
mechi zao kumalizika.
No comments:
Post a Comment