![]() |
|
Wananchi wa
Jiji la Mwanza wakiwa wamekaa kwa utulivu katika Mkutano wa
hitimisho la Chadema M4C Pamoja Daima ulifanyika katika Uwanja wa Furahisha
Jijini Mwanza Jioni ya Jana (Februari 01,2014).
|
![]() |
|
Chopa
iliyokuwa imembeba Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Wilbroad Slaa ikitua katika
Uwanja wa Furahisha ili aweze kuhutubia katika Mkutano wa Kampeni wa Chadema
M4C Pamoja Daima.
|
![]() |
|
Ze
nyomiziiiiiii ndani ya uwanjaa wa Furahishaaa wakisikiliza hotuba mbalimbali
kutoka kwa viongozi wa Chadema walioko kwenye Kampeni ya M4C Pamoja Daimaa.
|
![]() |
| Mbunge wa Nyamagana Mheshimiwa Ezekia Wenje akiwa na Matibu wa Chadema Taifa Bwan Mudi mwenye kombati ya Green na Mbungue wa Jimbo la Ilemela Mheshimiwa Highness Kiwia. |
![]() |
|
Mheshimiwa
Higness Kiwia akimpokea Bwana Darius Ngoko ambaye ameamua kuhama chama cha
Mapinduzi CCM na Kujiunga na Chadema katika Mkutano wa M4C Pamoja Daima.
|
![]() |
|
Mkurugenzi
wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasiana Maendeleo Chadema Bwana Wilfred
Mganyizi Lwakatare akitoa speecha yake ya kusalimia Mkutano wa M4C Pamoja Daima
katika viwanja vya Furahisha.
|
![]() |
|
Katika hali
ya kushangaza jeneza ambalo lilikuwa limechorwa picha ya aliyekuwa Naibu Katibu
Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe nalo lilionekana mbele ya Kamera kama
inavyoonekana.
|
![]() |
|
Katibu wa
Chadema Taifa Dr. Wilbroad Slaaa akihuthubia maelfu ya watanzania waliofurika
katika uwanja wa Furahisha Mwanza kusikiliza hitimisho la Kampeni ya M4C Pamoja
Daima jana Februari 01,2014.
|
![]() |
| Ze nyomiziiiiiii ndani ya uwanjaa wa Furahishaaa wakisikiliza hotuba mbalimbali kutoka kwa viongozi wa Chadema walioko kwenye Kampeni ya M4C Pamoja Daimaa. |
Pamoja na
mambo mengine katika mkutano huo,Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema
kimesema hakitalalamika tena kwa lolote au kukilamu Chama Cha Mapinduzi CCM
maana wameshaongea sana na sasa watafanya utekelezaji wa Ilani ya Chama chao.
Hayo
yamesemwa na Katibu wa Chama hicho Dr. Wilbroad Slaa katika hitimisho la
Kampeni za M4C Pamoja Daima lililofanyika jana Februari 01,2014 katika uwanja
wa Furahisha Mwanza.
Dr. Slaa
amesema kuwa wameshaongea kero mbalimbali za wananchi wa Tanzania lakini mpaka
sasa hakuna kilichofanyika hivyo wao kuanzia sasa wao kama Chadema
hawatalalamika zaidi ya kuchukua maamuzi ya utekelezaji tu.
Kampeni hizo
ambazo zimefanyika kwa siku 14 kwa kutembelea Majimbo yote ya upigaji kura ambayo
yalikua yamegawanyika katika makundi mawili kwa kutumia chopa tatu ambazo
zilikuwa zinaongozwa na Dr. Wilbroad Slaa, Freeman Mbowe na Tundu Lissu.


















No comments:
Post a Comment