Hawa ndio Wasanii hawa waliojiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho jijini Mbeya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 02, 2014

Hawa ndio Wasanii hawa waliojiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho jijini Mbeya.

Msanii JB akizungumza machace kwa niaba ya wenzake mara baada ya kutamka kuwa wamejiunga na chama cha Mapinduzi ( CCM) kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya.

Katibu wa NEC, Itikadi,na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye akiwatambulisha baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini,ambao kwa nia thabiti wameamua kujiunga na chama hicho,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB,Blandina Chagula,Mboto,Irene Uwoya,Single Mtambalike na wengineo.

Mwenyekiti wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshika jembe na nyundo,ikiwa ni alama ya Mkulima na Mfanyakazi mara baada ya kuwasili jioni ya leo kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya,Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuhudia tukio hilo. 

Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakifuatilia yanayojiri hivi sasa ndani ya uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine,mkoani Mbeya juu ya kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho.

Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,mara baada ya kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama cha CCM jioni ya leo Feb 02,2014. 

Kikundi cha TOT Plus kiongozwa na gwiji wa mipasho hapa nchini,Khadija Kopa wakiimba jukwaani.

Nape na wanachama wengine wakiserebuka kwa raha zao kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya.
 

Vijana wenye umri wa miaka 37 wakirusha njiwa angani kuashiria amani,utulivu na mshikamano wetu tulionayo.


 Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akipiga gitaa kabla ya kumzawadia msanii wa muziki maarufu wa jijini Mbeya,Petrol Abel a.k.a Awilo.

Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete  akimkabidhi zawadi ya gitaa Msanii maarufu wa jijini Mbeya,Petrol Abel a.k.a Awil,anaeshuhudia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi.Zakia Meghji. 
Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye sherehe hizo jioni ya leo Feb 02,2014 kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad