Taswira ya Timu ya Taifa ya netiboli ya Uganda ilivyochukua Ubingwa wa michuano ya Kombe la Mapinduzi 2014 huku soka Fainali Jumatatu kati ya Simba v KCC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 11, 2014

Taswira ya Timu ya Taifa ya netiboli ya Uganda ilivyochukua Ubingwa wa michuano ya Kombe la Mapinduzi 2014 huku soka Fainali Jumatatu kati ya Simba v KCC.


Mwenyekiti wa Baraza Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma kulia akimkabidhi Nahodha wa Uganda, Peace Proscovia Kombe la Mapinduzi ubingwa wa Netiboli 2014 jioni ya leo (Januari 11,2014) katika Uwanja wa Gymkhana, Zanzibar. Uganda iliifunga Tanzania Bara magoli 52-39.
Ushindi huo wa awali uliwapa morari wachezaji hao na kufanya hadi mapumziko kutoka kifua mbele kwa mabao 24-20.

Hadi mwamuzi anamaliza mchezo huo, Uganda ilikuwa kidedea kwa mabao 52-39 huku nahodha wao Peace akitwaa tuzo ya kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo.

Kufuatia ushindi huo, Mwenyekiti wa Baraza la wawakilishi, Mgeni Hassani Juma aliipatia timu hiyo kombe la michuano hiyo.

Licha ya Uganda kutwaa ushindi huo, Tanzania Bara chini ya mfungaji wake Mwanaidi Hassan ilitwaa nafasi ya pili ya michuano hiyo.

Mchezaji Bora wa michuano hiyo ni Betina Kazinja kutoka Tanzania Bara, Mwajuma Hilika kutwaa mlinzi bora wa michuano hiyo.


Peace Proscovia akidaka mpira mbele ya wachezaji wa Tanzania Bara…katika Uwanja wa Gymkhana, Zanzibar. Uganda iliifunga Tanzania Bara magoli 52-39.



Mwanaidi Hassan wa Tanzania Bara akidaka mpira pembeni ya wachezaji wa Uganda ambapo Uganda iliifunga Tanzania Bara magoli 52-39.



Sofia Komba alicheza sana leo(Januari 11,2014)  kujibu mapigo ya mpenzi wake, Joseph Owino aliyeifungia Simba SC bao jana(Januari 10,2014)  katika ushindi wa 2-0 kwenye soka dhidi ya URA ya Uganda.


Hongera rasta; Wachezaji wa Simba SC wakimpongeza mwenzao, Amri Kiemba kushoto baada ya kufunga bao la pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya URA ya Uganda katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi jana(Januari 10,2014) katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Aidha kwenye soka ,Mechi za Nusu Fainali, Azam FC walinyang’anywa Taji walipotupwa nje ya Mashindano ya Mapinduzi Cup, ambalo Mwaka huu ni kusheherekea Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, baada kuchapwa 3-2 na KCC ya Uganda iliyotinga Fainali na watakutana na Simba walioinyuka 2-0 URA ya Uganda.

Kwa Miaka miwili iliyopita, Azam FC wamekuwa Mabingwa wa Mapinduzi Cup.

Simba watacheza Fainali Jumatatu na KCC ambayo walikuwa nayo Kundi B kwenye Mashindano haya na kutoka 0-0 katika Mechi yao.

FAINALI MAPINDUZI CUP 2014.
Jumatatu Januari 13,2014.
Amaan Stadium

SAA 10 JIONI: Simba SC v KCC

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad