 |
|
Kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani Dodoma, nyumba 127
zimebomolewa na mafuriko ambapo watu 493 wamekosa makazi ya kuishi, pia nyumba
240 zimezingirwa na maji katika Kijiji cha Chipogolo Kata ya Chipogolo tarafa
ya Rudi Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma na kusababisha jumla ya wakazi 1390
kukosa makazi ya kuishi.
|
 |
|
Baada ya Mvua kunyesha :- Muuza Chipsi akiendelea kuandalia wateja wake huku maji machafu
yakiwa yametuama kibandani hapo eneo la standi ya Jamatini mkoani Dodoma hali inayotishia Afya za wateja wao, huku kilio
cha wafanyabiashara hao kikielekezwa ofisi ya mhandisi wa manispaa kwa
wanaotoza kodi.
|
 |
|
Maji yakiwa yamezagaa katika vibanda vya wafanya biashara wa chakula
(mama na baba lishe) kutokana na kukosekana na miundombinu ya kupitishi maji
pindi mvua zinaponyesha.
|
 |
|
Hii ni moja kati ya nyumba za polisi ambazo zimeharibiwa na mafuriko
hayo ambapo Naibu Waziri wa Nishati na madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Kibakwe Wilayani Mpwapwa Mh. George Boniface SimbaChawene amesema katika kikao
cha tathmini kilichofanyika mara baada ya kukagua eneo lililoathilika na
mafuriko, wamekubaliana hatua mbalimbali zichukuliwe ikiwemo kujenga upya
madaraja yaliyopo pamoja na kuongeza kimo na urefu wa madaraja hayo kwa kuwa
madaraja yaliyopo ni mafupi na yanazidiwa na maji.
|
 |
| Kituo cha Polisi Kata ya Chipogolo na nyumba tano za Askari
wa kituo hicho zimeanguka kutokana na mafuriko hayo, Kamanda Misime ametoa pole
kwa Askari wa kituo hicho na kuwasisitiza waendelee kufanya kazi kwa maadili ya
Jeshi bila kujali wakati tatizo lao linashughulikiwa na mamlaka husika kwani
vituo vya Polisi kama hivyo vipo chini ya Mkurugenzi na wananchi kwakuwa
vilijengwa kwa nguvu zao. |
Naibu Waziri wa Nishati na madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Kibakwe Wilayani Mpwapwa Mh. George Boniface SimbaChawene amesema katika kikao
cha tathmini kilichofanyika mara baada ya kukagua eneo lililoathilika na
mafuriko, wamekubaliana hatua mbalimbali zichukuliwe ikiwemo kujenga upya
madaraja yaliyopo pamoja na kuongeza kimo na urefu wa madaraja hayo kwa kuwa
madaraja yaliyopo ni mafupi na yanazidiwa na maji.
Pia Mbunge huyo ameiomba kamati ya maafa kufanya kila liwezekanalo
kuhakikisha kwamba wakazi wa kijiji hicho wanapata huduma mbalimbali zikiwemo
za Afya kwa kuwapa madawa, elimu pamoja na kuwaongezea wataalamu wa afya,
kuwapatia Mahema, mablaketi na magodoro na chakula.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mh. Christopher Ryoba Kangoye
amewaomba wakazi wa kijiji hicho kuendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki
kigumu wakati serikali kupitia kamati ya maafa Mkoa wa Dodoma ikiendelea
kushughulikias matatizo yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
David A. Misime amewataadharisha wakazi wa kijiji hicho kuwa watulivu kwani
matatizo kama haya hayatatuliwi kwa vurugu badala yake watumie vikao
vinavyostahili kutatua matatizo yao “matatizo kama haya hayatatuliwi kwa
kufanya fujo na kufunga barabara”
No comments:
Post a Comment