Taswira ya Sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar Januari 12,2014 na Jumatatu, Januari 13, 2014 ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 13, 2014

Taswira ya Sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar Januari 12,2014 na Jumatatu, Januari 13, 2014 ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa leo, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964 yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.  



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la heshima wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964 katika Uwanja wa Amani Abeid Karume Jana Januari 12, 2014.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la heshima wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Uwanja wa Amani Abeid Karume Jana Januari 12, 2014.

Vijana wakiachia njiwa kama alama ya amani wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Uwanja wa Amani Abeid Karume Jana Januari 12, 2014.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein wakimpongeza Rais Yoweri Kaguta Museveni aliyeongea machache wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Uwanja wa Amani Abeid Karume leo Januari 12, 2014.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein kwa hotuba nzuri aliyotoa  wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Uwanja wa Amani Abeid Karume leo Januari 12, 2014.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Yoweri Kaguta Museveni wakiongea  wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Uwanja wa Amani Abeid Karume Jana Januari 12, 2014.
(PICHA NA IKULU)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.

Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.

Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.  

Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.

Imetolewa na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
Ikulu,
Dar es Salaam.
Januari 12, 2014

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad