Haya ndio Matokeo ya Ligi Kuu Ulaya kwa Manchester City kukaa Kileleni,FC Barcelona kufungana Pointi 50 na Atletico Madrid huku Mabingwa watetezi na Vinara wa Serie A Juventus kileleni kwa pointi 52. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 13, 2014

Haya ndio Matokeo ya Ligi Kuu Ulaya kwa Manchester City kukaa Kileleni,FC Barcelona kufungana Pointi 50 na Atletico Madrid huku Mabingwa watetezi na Vinara wa Serie A Juventus kileleni kwa pointi 52.

Mshambuliaji wa Manchester City, Edin Dzeko (kulia) akimtungua kipa wa Newcastle, Tim Krul kuifungia bao la kwanza timu yake na Man City kurejea kileleni mwa Ligi Kuu Uingereza  baada ya kuichapa Newcastle kwa mabao 2-0. Awali Chelsea ndiyo ilishikilia uongozi huo kwa muda baada ya kufikisha pointi 46.

Dzeko na Negredo akaifungia City bao la pili dakika za majeruhi. ....................Ushindi huo unaifanya City irejee kileleni baada ya kutimiza pointi 47 kutokana na mechi 21, ikiishusha Chelsea yenye pointi 46 baada ya kucheza mechi 21 pia katika nafasi ya pili. Arsenal sasa ni ya tatu kwa pointi zake 45, ingawa imecheza mechi 20. 
Kikosi cha Alan Pardew kilidhani kimepata bao la kusawazisha baada ya shuti la mbali la Cheick Tiote kumpita kipa Joe Hart na kutinga nyavuni, lakini likakataliwa kwa sababu Yoan Gouffran alikuwa ameotea.

Luis Suarez akishangilia mbele ya wachezaji wenzake baada ya kufunga bao lake la pili na Daniel Sturridge wamendelea kucheza vizuri pamoja wakiisaidia Liverpool kuweka rekodi ya kushinda mechi ya kwanza Uwanja wa Stoke kwa zaidi ya miaka 29 baada ya kuwalaza wenyeji, Stoke City mabao 5-3.

Suarez alifunga mabao mawili dakika za 32 na 71 na kutimiza mabao 22 katika mechi 16 za ligi na Sturridge akafunga bao lake la 12 msimu huu dakika ya 87 akicheza kwa mara ya kwanza tangu Novemba 23, mwaka jana kutokana na kuwa nje kwa maumivu ya kifundo cha mguu. 

Mabao mengine ya Liverpool yalifungwa na Shawcross aliyejifunga dakika ya tano na Steven Gerrard dakika ya 51, wakati ya Stoke yalitiwa nyavuni na Peter Crouch dakika ya 39, Adam dakika ya 44 na Walters dakika ya 84.

Liverpool sasa inatimiza pointi 42 baada ya kucheza mechi 21 na kutulia nafasi ya nne, nyuma ya Asrenal yenye pointi 45, Chelsea 46 na Mancester City 47. 

Position Team Played Goal Difference Points
1 Man City 21 36 47
2 Chelsea 21 21 46
3 Arsenal 20 21 45
4 Liverpool 21 25 42
5 Everton 21 15 41
6 Tottenham 21 1 40
7 Man Utd 21 11 37
8 Newcastle 21 2 33
9 Southampton 21 4 30
10 Hull 21 -5 23
11 Aston Villa 20 -6 23
12 Stoke 21 -13 22
13 Swansea 21 -4 21
14 West Brom 21 -5 21
15 Norwich 21 -18 20
16 Fulham 21 -24 19
17 West Ham 21 -9 18
18 Cardiff 21 -19 18
19 Sunderland 21 -15 17
20 Crystal Palace 21 -18 17



Real Madrid, wakicheza Ugenini, Jana(Januari 12,2014) wameifunga Espanyol Bao 1-0 na kuzikaribia Timu mbili za juu kileleni, Barcelona na Atletico Madrid, ambazo zimefungana Pointi 50, na sasa kuwa Pointi 3 tu nyuma yao wakiwa na Pointi 47.

Bao la ushindi kwa Real lilifungwa na Beki Pepe kwa kichwa katika Dakika ya 55 alipounganisha Frikiki ya Luka Modric.
Kwenye Mechi hii, Cristiano Ronaldo, alikosa Bao 2 za wazi.

Jana Jumamosi(Januari 11,2014), Atletico Madrid na Barcelona zilitoka Sare ya 0-0 Uwanjani Vicente Calderon na kufungana kileleni wakiwa wote wana Pointi 50 lakini Barcelona wako mbele kwa ubora wa Magoli.



HUKO KATIKA LIGI YA ITALIA:-Mabingwa watetezi na Vinara wa Serie A huko Italy, Juventus, Jana (Januari 12,2014) wametoka nyuma kwa Bao 1 wakiwa Ugenini na kuitandika Cagliari Bao 4-1 na kuzidi kupaa kileleni wakiwa Pointi 8 mbele ya Timu ya Pili As Roma ambao nao leo waliikung’uta Genoa Bao 4-0.

Timu ya Nafasi ya Tatu, Napoli, wakicheza Ugenini, nao pia waliifumua Hellas Verona Bao 3-0 kwa Bao za Dries Mertens, Lorenzo Insigne na Blerim Dzemaili.

Kwenye Mechi ya AS Roma Genoa, Bao za AS Roma zilipachikwa na Alessandro Florenzi, Francesco Totti, Maicon Douglas Sisenando, Mehdi Benatia.

Mabingwa Juventus wajikuta wakipigwa Bao 1 na Cagliari katika Dakika ya 21 Mfungaji akiwa Mauricio Ferrera Pinilla ambae alipewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 87.

Juve walizinduka na kusawazisha Dakika moja baadae kwa Bao la Jose Martin Caceres na kuongeza Bao la Pili katika Dakika ya 31 kupitia Fernando Llorente.

Kipindi cha Pili, Juve walipiga Bao nyingine mbili za Claudio Marchisio, Dakika ya 73, na Bao jingine la Fernando Llorente katika Dakika ya 76.

MSIMAMO-KWA TIMU ZA JUU.

NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Juventus FC
19
17
1
1
46
12
34
52
2
AS Roma
19
13
5
1
39
10
29
44
3
SSC Napoli
19
13
3
3
41
20
21
42
4
Fiorentina
19
11
4
4
34
20
14
37
5
Hellas Verona
19
10
2
7
34
30
4
32
6
Inter Milan
18
8
7
3
37
22
15
31

RATIBA/MATOKEO 2013/2014.

Jumamosi Januari 11,2014.

Livorno 0 Parma 3
Bologna 0 Lazio 0

Jumapili Januari 12,2014.

Torino 0 Fiorentina 0
AS Roma 4 Genoa 0
Atalanta 2 Calcio Catania 1
Cagliari Calcio 1 Juventus 4
Hellas Verona 0 SSC Napoli 3
Sassuolo Calcio 4 v AC Milan 3

Jumatatu Januari 13,2014.

21:00 Sampdoria v Udinese
23:00 Inter Milan v Chievo Veron
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad