|
Mjane wa Dr Mgimwa akiaga mwili
huo kabla ya mazishi kijiji cha
Magunga mkoani Iringa yaliyofanyika leo(Januari 06,2014) jimbo la Kalenga.
|
| Mwili wa Dr Mgimwa ukishushwa kaburini leo(Januari 06,2014) jimbo la Kalenga. |
|
Rais Kikwete na mkewe wakiweka
shada la maua Katika mazishi hayo
yaliyofanyika leo kijiji kwake Magunga
jimbo la Kalenga .
|
|
Waziri Mkuu
Pinda alisema kuwa
serikali imepata pigo kubwa juu
ya kifo hicho na kuwa bado serikali itaendelea
kuwa karibu na familia ya Dr Mgimwa
na pale penye tatizo isisite
kuwasiliana .
|
Maelfu ya
wakazi wa mkoa wa Iringa na
baadhi ya viongozi
wa vyama vya
siasa na Serikali wakiongozwa na Rais Dr
Jakaya Kikwete wameshiriki
katika mazishi ya aliyekuwa mbunge wa
jimbo la Kalenga na waziri wa
fedha Dr
Wiliam Mgimwa.
Huku waziri
mkuu Mizengo pinda katika salam
zake za serikali akielezea jinsi
ambavyo Taifa lilivyopata
pigo kubwa kufuatia kifo
cha Dr Mgimwa kutokana na mchango
wake katika baraza la mawaziri.
Katika mazishi
hayo yaliyofanyika leo kijiji
kwake Magunga jimbo la
Kalenga wananchi mbali
mbali walionyesha kujipanga
barabarani kutoka Manispaa
ya Iringa hadi
kijijini kwake huku wakiupungia mkono msafara wa
rais Kikwete na baadhi yao
wakilazimika kutumia usafiri wa baiskeli na pikipiki kwenda katika mazishi hayo.
Akitoa shukrani za
familia kwa niaba ya familia mtoto wa marehemu Dr Mgimwa Godfrey Mgimwa
aliishukuru serikali kwa jinsi ambavyo ilivyohangaika kumuuguza baba yake
na kutoa wosia mzito wa marehemu Dr Mgimwa ambao alimtaka kuufikisha kwa Rais Kikwete..
Alisema katika
uhai wake kabla ya kifo
chake ikiwa ni siku tano
kabla Dr
Mgimwa alimwita na kumtaka kufikisha
shukrani zake kwa Rais Kikwete
kwa kumtembelea mara mbili Hospital alipokuwa amelazwa pamoja na
spika wa bunge Anne makinda .
Pia alisema
kuwa alieleza dhamira yake
ya kuwatumikia wana Kalenga na kusema
zawadi kubwa ni msaada wa bati
zaidi ya 2000 kwa wananchi hao ili kuendeleza ujenzi wa shule na vituo
vya afya jimboni.
"Baba kabla ya
kufa aliniachia wosia
huo juu ya wana Kalenga kwa kuwashukuru kwa ushirikiano
wao na kutoa bati ila alipenda kuona
Kalenga inakuwa na maendeleo
zaidi"
Kwa upande
wake waziri Mkuu Pinda alisema
kuwa serikali imepata pigo
kubwa juu ya kifo hicho na kuwa bado serikali
itaendelea kuwa karibu na familia
ya Dr Mgimwa na pale penye tatizo
isisite kuwasiliana .
Hata hivyo
Rais Kikwete hakupata
kuzungumza chochote katika msiba
huo zaidi ya kuweka mchanga na shada la maua pamoja na
kuwapa mkono ndugu wa Dr Mgimwa .
Spika wa bunge Anne Makinda alisema kuwa
bunge limempoteza kiongozi na
mbunge aliyependa kutumia nafasi yake
kwa ajili ya Taifa na kuwa kamwe
mchango wake hawataacha kuukumbuka.
PICHA NA HABARI KWA
HISANI YA FRANSIS GODWIN IRINGA.





No comments:
Post a Comment