![]() |
|
Asikari wa
usalama barabarani akiwa karibu na Gari hilo baada yakuondolewa toka kwenye
gema lililoinusuru isitumbukie chini ya Daraja ilipotokea ajali hiyo.
|
Kamanda wa Kikosi cha Reli Tanzania, Bi.Saada Haji anasema kwamba jumla ya ajali 79 zinazohusisha treni zilitokea mwaka jana(2013) katika mikoa tofauti nchini Tanzania.
Alisema kuwa
hata hivyo ajali nyingi kati ya hizo zimetokana na uzembe, ikiwemo kulewa na
kukaa juu ya reli, kuweka ‘headphone’ na kutembea relini na madereva wa magari
kukosa umakini wa kufuatilia alama za barabarani kwa kuendesha mwendo kati hata
mahali penye kivuko cha treni.
“ Treni
linalofanya safari zake ndani ya jiji ndiyo ambalo kwa sasa linahisisha vifo
vya watu wengi kwa muda mfupi tangu kuanza kwa safari zake watu 8 wamekufa huku
wengine wakijeruhiwa,” alisema Kamanda Haji.
Alisisitiza”
Hasa katika eneo la Daraja la Buguruni kwa Mnyamani ndiyo eneo ambalo ni
hatari, kwani limekuwa na matukio ya ajali, wananchi wengi hujisahau
hukatiza juu ya reli kwa kuwa treni huwa halina breki za papo kwa papo basi
vifo au majeraha makubwa yanayowasababishia ulemavu wa kudumu,”
Akizungumzia
kuhusu matukio 285 ya uhalifu alisema kuwa yalitokea katika mikoa ya
Morogoro, Dodoma, Itigi, Tabora, Mwanza, Kigoma, Mpanda na Dar es Salaam,
ambayo yaliyokea katika maeneo ya reli na ndani ya treli.
“ Polisi wa
kikosi hiki wamekuwa wakipambana kikamilifu, kuna siku walifanikiwa kukamata
mabegi yaliyowekea bangi, ambapo mtuhumiwa alifikishwa mahakamani ",
alisema.
Alisema kuwa Polisi hao pia waliwahi kumbaini mhalifu mmoja aliyekuwa na amebeba silaha isivyo halali ndani ya treni ambaye alikurupuka na kuitelekeza siraha hiyo









No comments:
Post a Comment