Tuhuma hizo
ni pamoja na:-
1. Kwamba
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa mwaka 2005 eti alichukua fedha kutoka kwa Mbunge wa
Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kiasi cha sh.Milioni 40 ili Mwenyekiti
Mbowe asifanye kampeni katika jimbo hilo.
2. Mwaka
2008, eti Mbunge Mkono alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa, sh. Milioni 20 kwa
ajili ya uchaguzi mdogo wa Tarime, kisha akazitoa kwenye chama kama mkopo na
akalipwa.
3. Mwaka
2010, wakati wa uchaguzi mkuu Mbunge Mkono eti alimpatia Mwenyekiti wa Chama
Taifa sh. Milioni 200 kwa ajili ya kampeni za mgombea urais.
4. Mwaka huo
huo wakati wa uchaguzi mkuu, eti Mwenyekiti wa Chama Taifa, alipokea sh.
Milioni 100 kutoka kwa Rostam Aziz kwa ajili ya kampeni.
Idara ya
Habari ya CHADEMA, inapenda kutaarifu umma yafuatayo:-
1. Hakuna ukweli
hata mmoja katika tuhuma hizo.
Ni uongo na uzushi uliopangiliwa kama moja ya
mikakati ya watu wenye malengo ya kutaka kuilaghai jamii kwamba viongozi wa
CHADEMA hawana tofauti na wale wa CCM na kwamba chama hiki kikuu cha upinzani
kinachobeba matumaini ya Watanzania katika kupigania haki zao na kupinga kila
aina ya ufisadi, kionekane hakina tofauti na chama kilichoko madarakani,
ambacho kimepoteza ushawishi kwa wananchi.
2. Matokeo
ya uongo huo ni kutaka kuisaidia CCM na kugeuza mjadala.
3. Idara ya Habari
ya CHADEMA inapenda kuuambia umma wa Watanzania wote, hususan wanachama,
wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda mabadiliko nchini kwamba,Mwenyekiti wa
Chama Taifa, ameshawasiliana na mawakili walifanyie kazi suala hili kwa ajili
ya kuchukua hatua za kisheria.
4. Kwa
uhakika tunapenda kuiambia jamii ya Watanzania wote, hususan wanachama,
wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda mabadiliko wote nchini, kwamba; Chama
wala Mwenyekiti wa Chama Taifa, mahali popote na wakati wowote, hajawahi
kupokea msaada wa fedha hizo kutoka kwa waliotajwa kwa malengo yaliyosemwa.
5.
Tungependa kuwaambia waliozusha tuhuma hizo, ni vyema kama wanapenda kutunza
heshima kidogo waliyobakiza katika jamii kutokana na kuelemewa na mzigo wa
tuhuma za utovu wa maadili na usaliti dhidi ya CHADEMA, badala ya kugeuka kuwa
mabingwa wa kupika uongo, wajibu masuala ya msingi yanayowaandamana kuhusu
mikakati yao ya kuhujumu CHADEMA na viongozi wake, ambayo iwapo chama
kisingeibaini na kuchukua hatua za kinidhamu, ingesababisha kuua ndoto na
matumaini ya Watanzania kufanya mabadiliko ya kimfumo na kiutawala, kwa
kuiondoa CCM madarakani.
6. Taarifa
kuhusu baadhi ya tuhuma katika mkakati huo ambazo zimemlenga Mwenyekiti wa
Chama Taifa, kwa kuhusisha shughuli zake binafsi za uwekezaji, zitajibiwa
kupitia taasisi husika.
Imetolewa
leo Dar es Salaam na;
Tumaini
Makene
Ofisa
Mwandamizi wa Habari- CHADEMA






No comments:
Post a Comment