KCC ya
Uganda leo(Januari 13,2014) huko Amaan Stadium, Zanzibar wametwaa Mapinduzi Cup, moja ya Sherehe
mahsusi kusheherekea Miaka 50 ya Mapinduzi matukufu, baada kuitungua Simba Bao
1-0.
Shujaa wa
KCC ni Herman Wasswa aliefunga Bao pekee la Fainali hii katika Dakika ya 20
baada kupokea Krosi kutoka Habib Kavuma na kumtambuka Beki Mkenya Donald Musoti
na kumchambua Kipa Ivo Mapunda.
Hii ni mara
ya pili kwa KCC na Simba kukutana kwenye michuano hiyo baada kutoka 0-0 katika
hatua za Makundi na hii ni mara ya kwanza kwa Simba, inayofundishwa na Kocha
toka Serbia Zdravko Logarusic, ‘kutobolewa’ kwa Bao katika Mashindano hayo.
Mbali ya
kunyakua Kombe, KCC pia wamezoa zawadi ya Dola 10,000 kama Mabingwa.
Kwenye
Ufungaji Bora, Kiungo wa URA, Owen Kasule, alitwaa Tuzo ya Ufungaji Bora akiwa
na Bao 4 na Herman Wasswa, wa KCC, na Amri Kiemba, wa Simba, wanafuatia wakiwa
na Bao 3.






No comments:
Post a Comment