SIRI nzito
imevuja! Ni dhahiri kwamba, Rais Jakaya Kikwete ‘JK’ hatavunja baraza la
mawaziri kufuatia kusitisha kwake uteuzi wa mawaziri wanne na kifo cha
aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi,
Dk. William Augustao Mgimwa kama wengi wanavyoamini bali atabadilisha
tu, Risasi Jumamosi lina cha kushika mkononi.
Mawaziri
ambao uteuzi wao ulitenguliwa ni Emmanuel John Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi
Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Mathayo David Mathayo
(Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) na Balozi Khamis Juma Kagasheki (Maliasili na
Utalii) aliyejiuzulu kutokana na ukiukwaji wa maadili na haki za binadamu
katika Oparesheni Tokomeza Ujangili.
![]() |
|
Waziri Mkuu
wa Tanzania , Bw.Mizengo Pinda.
|
KWA NINI
HAVUNJI BARAZA?
Kwa mujibu
wa chanzo cha ndani serikalini, JK hana mpango huo kwa sababu kuu mbili. Kwanza
kuvunja baraza la mawaziri ni kumuweka kando waziri mkuu wa sasa, Mizengo
Kayanza Peter Pinda na kuteua waziri mkuu mwingine.
Pili,
atakuwa anaongeza mzigo kwa serikali kwa
kuwa waziri mkuu akiondoka madarakani huendelea kulindwa na serikali na kupokea
stahiki zake mbalimbali.
![]() |
|
Waziri wa
sasa wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw.Shukuru Kawambwa.
|
NI HAYATI NYERERE.
Tangu
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ni Baba wa Taifa tu, hayati Mwalimu Julius
Nyerere ndiye aliyewahi kuwa na mawaziri wakuu wanne.
Alianza na
Rashid Mfaume Kawawa, akafuata Edward Moringe Sokoine, Salim Ahmed Salim (baada
ya kifo cha Sokoine) na Cleopa David Msuya.
AWAMU YA
RAIS MWINYI.
Katika awamu
ya pili, Rais Ally Hassan Mwinyi, mawaziri wakuu walikuwa Joseph Warioba, John
Malecela na David Msuya.
Katika awamu
ya tatu ya Rais Benjamin William Mkapa kulikuwa na waziri wakuu mmoja tu,
Frederick Tuluwayi Sumaye.
![]() |
| Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, mama Anne Kajumulo Tibaijuka. |
WAZIRI MKUU
HADI 2015.
Kwa sababu
hiyo, chanzo kikasema kuwa Pinda ataendelea ‘kuula’ kwenye nafasi yake ya kuwa
waziri mkuu wa Tanzania hadi mwisho wa muhula wa awamu ya nne, mwaka 2015.
WATAENDELEA
KUPANGUA.
Hata hivyo,
kwa mujibu wa chanzo hicho, JK na rais ajaye wataendelea kukumbwa na shinikizo
la kupangua baraza la mawaziri kila wakati kutokana na mfumo wa madaraka uliopo
sasa.
“Unajua
mfumo wa sasa uko hivi; waziri anateuliwa na rais, katibu mkuu wa wizara pia
anateuliwa na rais.
Katibu mkuu wa wizara ana uwezo wa kumfukuza kazi
mkurugenzi wa halmashauri bila waziri kujua, lakini waziri hana uwezo huo.
“Nguvu kubwa
ya kazi ipo kwa makatibu wakuu ambao ndiyo watendaji wakubwa wa wizara.
Kinachotokea ni kwamba kama wizara itampata waziri mwenye kusimamia sawa
majukumu yake kiasi cha kutishia ulaji wa makatibu wakuu, atawekewa zengwe
mpaka ang’oke.
“Ndiyo maana
utakuta mawaziri kwenye wizara kila siku wanawajibika kisiasa lakini makatibu
wakuu wapo tu.
Ni mfumo mbaya wa kimadaraka hivyo JK atabadili kila siku, hata
rais ajaye naye atakuwa katika harakati hizo,” kilisema chanzo hicho.
MAWAZIRI
ZAIDI.
Chanzo
kikaenda mbele zaidi kwa kunyetisha kwamba, wapo mawaziri ambao wanakalia kuti
kavu na huenda wakang’olewa kabisa kutokana na utendaji kazi wao usioridhisha.
![]() |
| Bw.Shukuru Kawambwa. |
SHUKURU
KAWAMBWA.
Huyu
anadaiwa kung’oka wakati wowote kutokana na madai ya walimu.
Chanzo
kilisema kuwa Kawambwa pia anaponzwa na mfumo kwani kwa kawaida mwalimu
anaajiriwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi lakini usimamizi wake
unakuwa chini ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Ikadaiwa
kuwa mwalimu anapandishwa cheo na Wizara ya Utumishi, lakini mshahara analipwa
na Wizara ya Fedha, Mipango na Uchumi (hazina).
“Sasa
mwalimu akipandishwa cheo na utumishi, nyongeza ya mshahara inatakiwa itoke
hazina.
Hazina nao wanakuwa hawana habari kwa sababu ya mawasiliano duni,
matokeo yake mwalimu analia na mwajiri wake ambaye ni Wizara ya Elimu. Hili la
walimu litamng’oa Kawamba,” kilisema chanzo.
WAZIRI ANNA
TIBAIJUKA.
Chanzo
kilidai kwamba Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, mama Anne Kajumulo
Tibaijuka naye yupo mguu pande, sawa kwa sababu ya migogoro ya wakulima na
wafugaji.
Mfano:
“Wakulima wanaopakana na Kiwanda cha Mbolea cha Minjingu, Manyara, wamekuwa
wakilalamikia kitendo cha mazao yao kuunguzwa na mbolea hiyo, waziri
ameshaambiwa akajibu atafuatilia, sasa atafuatilia mpaka lini?
Waziri wa
Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza.
“Kuna kamati
iliundwa kufuatilia suala hili. Pia inadaiwa kuwa vigogo mbalimbali wa serikali
wamejimegea maeneo makubwa ya ardhi mkoani Morogoro hivyo kusababisha migogoro
isiyoisha kati ya wakulima na wafugaji wanaogombea ardhi kiduchu iliyobaki,
huenda ikawa miongoni mwa mambo yatakayomng’oa madarakani Mheshimiwa
Tibaijuka,” kilisema chanzo.
![]() |
| Add caption |
WAZIRI CHRISTOPHER CHIZA.
Huyu ni
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika. Wizara yake inakabiliwa na tuhuma ya
kuzembea kwenye eneo la mashamba ya mpunga katika Kijiji cha Kapunga, Mbarali,
Mbeya.
“Kuna kaburu
mwekezaji alinunua shamba hilo lililokuwa la Nafco, hajalilima matokeo
yake analikodisha kwa wanakijiji
vipandevipande.
Sasa mtu ataitwaje mwekezaji wakati ni mbangaizaji tu, hii ni
kashfa, wizara ipo na haisemi lolote.
“Naamini
ripoti ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyokuwa ikiongozwa na Profesa
Peter Msolwa itaanika madudu yote haya,” kilisema chanzo.
WANAVYOTAKA
WANANCHI WA TANZANIA.
Kwa mujibu wa Risasi
Jumamosi wiki iliyopita liliingia mitaani kusikiliza maoni ya wananchi juu ya
watu wanaotakiwa kuwa mawaziri kushika nafasi zilizoachwa wazi.
Katika kila
wananchi kumi, nane walitaka mawaziri na wizara zao wawe hivi:-
Benard
Membe, Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi.
Asha-Rose Mtengeti Migiro (Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), Lazaro Samuel Nyalandu (Waziri wa
Maliasili na Utalii) na Anne Kilango Malecela (Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na
Uvuvi).
Wananchi hao
walisema, Harrison George Mwakyembe na John Pombe Magufuli waendelee kwenye
wizara zao kwa vile utendaji kazi wao ni
mzuri, hauna shaka huku wakitaka George Huruma Mkuchika awe Waziri wa Ulinzi.
“Ila Amos
(Gabriel) Makalla awe waziri kamili wa habari, yule mama (Fenella Mukangala)
apelekwe wizara nyingine.
Waziri wa Mambo ya Ndani sisi wananchi tunamwona.
Halafu yule mama anaitwa Joanista (Joackim) Mhagama aingizwe kwenye Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,” alisema mkazi wa Kijitonyama, Dar
aliyejitambulisha kwa jina la Kadoda, fundi wa magari, Bamaga, Mwenge.
Source: GPL












No comments:
Post a Comment