Mabingwa watetezi wa Ligi Yanga SC wameshushwa kileleni na kuipisha Azam FC kileleni kwa kufikisha Pointi 33 baada ya kuifunga Rhino Rangers bao 1-0 . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, January 29, 2014

Mabingwa watetezi wa Ligi Yanga SC wameshushwa kileleni na kuipisha Azam FC kileleni kwa kufikisha Pointi 33 baada ya kuifunga Rhino Rangers bao 1-0 .


Kocha mkuu wa Yanga SC Hans van der Pluijm ameishusha kileleni Yanga SC baada ya mechi mbili tu za Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara na Huo unakuwa mchezo wa nne kwa Yanga SC kucheza chini ya kocha wake mpya, ikishinda mechi mmoja tu.


Timu ya Azam FC Leo (Januari 29,2014)  imeitoa Yanga SC kwenye kilele cha Ligi kuu soka Vodacom Tanzania bara (VPL) ilipoifunga Rhino Rangers ya Tabora Bao 1-0 huko Azam Complex na Yanga SC kutoka Sare ya 0-0 na Coastal Union huko Mkwakwani Jijini Tanga.

Kocha mkuu wa Yanga SC Hans van der Pluijm ameishusha kileleni Yanga SC baada ya mechi mbili tu za Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara na Huo unakuwa mchezo wa nne kwa Yanga SC kucheza chini ya kocha wake mpya, ikishinda mechi mmoja tu.

Awali Mholanzi huyo aliyefukuzwa fukuzwa timu kibao Ghana na St George ya Ethiopia kwa matokeo mabaya kabla ya kutua Jangwani, alitoa sare mbili katika ziara ya Uturuki na akashinda dhidi ya Ashanti United kwa taabu 2-1 (Januari 25,2014) Jumamosi katika Ligi Kuu.

Katika mchezo wa leo uliotawaliwa na vurugu za mashabiki.


Huko Mabatini, Mlandizi, Ruvu Shooting na Mbeya City zilitoka Sare ya Bao 1-1 kwenye Mechi ambayo Ruvu walifunga mwanzo katika Dakika ya 4 kwa Bao la Jerome Lambele na Mbeya kusawazisha Dakika 9 baadae kupitia Jeremiah John.

Matokeo yameifanya Azam FC ishike usukani ikiwa na Pointi 33, Yanga SC Nafasi ya Pili, Pointi moja nyuma na Mbeya City wako nyuma ya Yanga kwa Pointi 1 huku Timu zote zimecheza Mechi 15.

RATIBA/MATOKEO VPL 2013/2014.

Jumatano Januari 29,2014.

Kagera Sugar 0 v Mtibwa Sugar 0
Azam FC 1 Rhino Rangers 0
Ruvu Shooting 1 Mbeya City 1
Coastal Union 0 Yanga 0

RATIBA VPL 2013/2014.

Jumamosi Februari 1,2014.

Ashanti United v Mgambo JKT [Azam Complex, Dar es Salaam]
Simba v JKT Oljoro  [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]

Jumapili Februari 2,2014.

Yanga SC v Mbeya City [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]

MSIMAMO WA LIGI KWA SASA.

NO
TEAMS
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Azam FC
15
9
6
0
25
10
15
33
2
Young Africans
15
9
5
1
33
12
21
32
3
Mbeya City
15
8
7
0
22
12
10
31
4
Simba SC
14
7
6
1
27
13
14
27
5
Kagera Sugar
14
5
5
4
15
11
4
20
6
Mtibwa Sugar
14
5
5
4
19
18
1
20
7
Coastal Union
15
3
9
3
11
8
3
18
8
Ruvu Shootings
14
4
6
4
16
16
0
18
9
JKT Ruvu
14
6
0
8
13
18
-5
18
10
Rhino Rangers
15
2
5
8
9
18
-9
11
11
JKT Oljoro
14
2
5
7
10
11
-10
11
12
Ashanti United
14
2
4
8
13
26
-13
10
13
Tanzania Prisons
13
1
6
6
6
16
-10
9
14
Mgambo JKT
14
1
3
10
5
26
-21
6

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad