![]() |
Gari la
Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja wa MSD Kanda pamoja na Waandishi wa Habari.
|
![]() |
Gari la
Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja wa MSD Kanda pamoja na
waandishi wa habari na hapo ni Askari akilikagua gari hilo.
|
Meneja wa
Boharia ya Dawa (MSD) Kanda ya Ziwa pamoja na waandishi watatu wa habari
wamenusurika kufa baada ya gari walilokuwa wakitumia katika msafara Rais Jakaya Kikwete mkoani Geita kupinduka.
Ajali hiyo
imetokea leo eneo la Nyankumbu kata ya Kalangalala, majira ya saa 3:54 asubuhi,
wakati gari aina ya Toyota Land Cruiser, lilipopinduka muda mfupi wakati
msafara wa Rais Kikwete ulipoanza safari kuelekea wilayani Nyang’wale kwa
ziara.
Walionusurika
katika ajali hiyo ni mwandishi Peter Fabian wa Gazeti la Rai, Frederick
Katulanda Moderator wa www.mabadiliko.com, Peter Makunga wa Radio Free Afrika,
meneja wa MSD kanda ya Ziwa Byekwaso Tabura pamoja na dreva wa gari hilo Yungi
Mkwati.
Akizungumza
baada ya tukio hilo, Meneja Tabura alieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni
utelezi wa Lami iliyokuwa umewekwa juu ya tuta la Barabara ya moramu
inayoendelea kujengwa, hali iliyosababisha gari hili kupoteza mwelekeo na
kuacha njia na kupinduka.
“Hii
barabara ambayo msafara unapita ipo katika matengenezo, inawekewa Lami,
inaonekana wakandarasi hawa waliamua kumwaga lami rojo ili kwa ajili ya kuja
kuweka kokoto, hivyo barabara ilikuwa ikiteleza, ndicho chanzo cha ajali yetu,”
alieleza Tabura.
Mganga
mfawidhi wa Hospitali ya Geita, Dk. Adam Sijaona alieleza kuwa wahanga wa ajali
hao walipokelewa Hospitalini hapo na kuchunguzwa afya zao, wanne kati yao
waliruhusiwa kuendelea na shughuli zao, lakini mmoja tuliamua kumpumzisha kwa
muda kutokana na kuwa na maumivu makali ya mkono wa kulia.







No comments:
Post a Comment