Hii ndio Taswira ya Ufukuaji wa Makaburi ili kupisha Ujenzi wa Kizuizi cha mpaka kati ya Nchi ya Tanzania na Burundi katika Eneo la Nzanza Kata ya Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, November 04, 2013

Hii ndio Taswira ya Ufukuaji wa Makaburi ili kupisha Ujenzi wa Kizuizi cha mpaka kati ya Nchi ya Tanzania na Burundi katika Eneo la Nzanza Kata ya Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera.

Zoezi la kuhamisha makaburi  40 kutoka katika eneo la ujenzi wa kizuizi cha mpaka baina ya nchi ya Tanzania na Burundi ,katika eneo la Nzaza kata ya Kabanga wilayani Ngara Mkoani Kagera limefanyika leo(Novemba 04,2013) na miili ya Ndugu pamoja na Jamaa kuzikwa upya kutoka eneo hilo....Picha na Mdau Shaabani Ndyamukama-Ngara.

Diwani wa kata ya Kabanga Bw Said Soud amesema kuwa zoezi hilo limefanyika kwa amani na kwamba mabaki ya miili 36 ilikuwa imepatikana na kuchukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya mazishi na kwamba Wanafamilia wa marehemu hao wameonyesha ushirikiano wa kutosha, licha ya  kuwepo changamoto za matumizi ya vifaa duni  vya kuchimbulia makabuli na kubeba miili ya ndugu zao.

Katika  zoezi hilo wananchi waliokuwa wamesusia kuhamisha makaburi ya ndugu zao na kuzuia makampuni yanayofanya kazi ya ujenzi wa kizuizi hicho sasa wameungana pamoja baada ya kukubali viwango vya fidia.

Wakiongea na Waandishi wa Habari katika eneo hilo wananchi wamesema serikali imefanya jambo la maana kuwapatia fidhia ya fedha za kuhamisha makaburi hayo na kuzikwa upya kwa ndugu zao.
Tumepata wakati mugumu kwani miili mingine ilikuwa ni ya siku za hivi karibuni hivyo kuogopa kuifumua na kuleta madhara wakati wa kuihamishia kwenye majeneza mapya”.Alisema Niyonzima  Marchades 
Katika hatua nyingine, Diwani wa Kata ya Kabanga Bw Said Soud amewataka wakazi wa kata ya Kabanga kutoa ushirikiano katika zoezi la kujenga kizuizi hicho kupitia  kampuni ya ujenzi ya Lukolo Co.LTD.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad