Hivi ndivyo Jeshi la Polisi mkoani Mwanza,lilivyowashikilia Waganga wa Jadi wawili baada ya kukamatwa wakiwa na kiungo cha binadamu wakitaka kukiuza kwa sh. milioni 100. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, November 05, 2013

Hivi ndivyo Jeshi la Polisi mkoani Mwanza,lilivyowashikilia Waganga wa Jadi wawili baada ya kukamatwa wakiwa na kiungo cha binadamu wakitaka kukiuza kwa sh. milioni 100.

Waganga hao  wawili wa jadi akiwemo mfanyabiashara mmoja walinaswa jijini Mwanza (October 28,2013) saa tisa alasiri eneo la Ziwani jirani na Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Manispaa ya Ilemela,wakiwa na kiungo cha mkono wa kulia unaoamainika kuwa wa binaadamu ,kufatia taarifa za raia wema na kisha jeshi la polisi kuweka mtego kwa muda wa wiki nzima na kufanikiwa kuwakamata.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza  alithibitisha tukio hilo na kwamba mkono huo uliokuwa umewekwa kwenye begi ukiwa umefungwa kwenye mfuko mweusi wa plasitiki na kuviringishwa kwenye karatasi nyeupe ya nailoni, umekutwa ukiwa mbichi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Upelelezi Makosa ya Jinai (RCO), ambaye pia ni Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Joseph Konyo, alisema watuhumiwa walikamatwa baada ya kufuatiliwa na polisi.

Watuhumiwa hao (majina yanahifadhiwa)
wenye umri wa miaka 36 na 43
(ni waganga wa jadi wawili) na
mfanyabiashara ana miaka 48.
"Oktoba 20 mwaka huu, tulipata taarifa za mtu mmoja kujihusisha na biashara ya viungo vya binadamu, eneo la Igombe, Manispaa ya Ilemela...tulimtuma mtu wetu ili akafanye manunuzi ya viungo hivyo, kutoka kwa mganga mmoja (jina linahifadhiwa).

"Hivi karibuni tulifanya vikao na waganga wa jadi kuzungumzia umuhimu wa kushirikiana na kupeana taarifa za kubaini waganga wanaopiga ramli chonganishi na wakata mapanga lengo likiwa ni kukomesha mauaji ya vikongwe," alisema.

Alisema baada ya vikao hivyo, walipokea taarifa kuwa mganga wa jadi huko Igombe anauza viungo vya binadamu na kuweka muda maalumu wa kutoa kichwa cha binadamu, mkono, nyeti.

Mganga huyo alizungumza na mteja (polisi), wakutane ili wafanye biashara akidai yupo na wenzake wawili wakiwa na begi ambapo mganga huyo alitaka apewe sh. milioni 100 lakini mteja aliomba apunguziwe bei na kuwaweka watu hao chini ya ulinzi.

"Baada ya begi lao kupekuliwa, kulikutwa chungu ambacho ndani yake kulikuwa na mfuko wa plastiki uliokuwa na kiganja cha mkono wa kuume wa binadamu kikiwa hakijaharibika.


Konyo alikataa kutaja majina ya watuhumiwa kwa madai ya kuvuruga upelelezi, kwani bado wanamtafuta mfanyabiashara mmoja jijini humo ambaye ametajwa na watuhumiwa kuwa anajihusisha na biashara hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad