Hatimaye Mwli wa Dk.Sengondo Mvungi waagwa Jijini Dar es Salaam. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, November 16, 2013

Hatimaye Mwli wa Dk.Sengondo Mvungi waagwa Jijini Dar es Salaam.

Jeneza la mwili wa Marehemu likiwa limewasili viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo..Novemba 16,2013.
 Dk Mvungi alifariki dunia, Jumanne iliyopita kwenye Hospitali ya Milpark Johannesburg, Afrika Kusini baada ya kuumizwa na watu wasiojulikana waliomvamia nyumbani kwake, usiku wa Novemba 2 mwaka huu.
...Watoto wa marehemu Dorine na Neema. ...
...Mke wa marehemu akiwa na mtoto wake wa kiume.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Dkt.Sengondo Mvungi, likiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee.
...Watoto wa marehemu wakitoa heshima ya mwisho wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
...Mmoja wa mtoto wa marehemu wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo .
...Watu mbalimbali wakiendelea kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo .
...Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda  akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
...Baadhi ya wanasheria wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo. .(Novemba 16,2013).
...Mkurugenzi wa kampuni ya IPP Media Reginard Mengi(kushoto) na Prof.Ibrahim Lipumba(katikati) Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
...Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Katiba Jaji Joseph Sinde Warionba akiongea machache wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
...Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza kutoka salamu za rambi rambi za serikali wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
...Makamu wa Rais Dkt Gahlib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Katiba Jaji Joseph Warioba, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mhe Angela Kairuki na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe James Mbatia wakiwa katika shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi.

( PICHA: SHAKOOR JONGO, RICHARD BUKOS NA DENIS MTIMA/GPL )

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad