Wekundu wa Msimbazi Simba SC waikung’uta wauza mitumba Ashanti United mabao 4-2. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, November 06, 2013

Wekundu wa Msimbazi Simba SC waikung’uta wauza mitumba Ashanti United mabao 4-2.

Said Ndemla akimpongeza
 Mombeki baada ya kufunga.
Wekundu wa Msimbazi Simba SC imezinduka jioni ya leo(November 06,2013) baada ya kucheza mechi nne bila kushinda, ikiibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Ashanti United ya Ilala, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Simba SC kumbuka ilitoka sare tatu dhidi ya Yanga SC  (3-3), Coastal Union (0-0) na Kagera Sugar (1-1) na kufungwa 2-1 na Azam FC.

Simba SC leo ilipata ushindi wake kupitia kwa Betram Mombeki aliyefunga mawili, Amisi Tambwe na Ramadhani Singano ‘Messi’.

Pamoja na ushindi huo, Simba SC inabaki nafasi ya nne kwa pointi zake 24, baada ya kucheza mechi zote 13 za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu.

Azam FC na Mbeya City zina pointi 26 kila moja na Yanga inafuatia kwa pointi zake 25 na timu zote hizo zitacheza mechi zake za mwisho kesho(November 07,2013).

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Andrew Shamba wa Pwani, hadi mapumziko tayari timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1.

Simba SC walitangulia kupata bao dakika ya nane kupitia kwa winga wake machachari, Ramadhani Singano ‘Messi’ aliyepasua katikati ya ukuta wa Ashanti baada ya pasi ya Amisi Tambwe kabla ya kumchambua kipa mkongwe, Amani Simba.


Mshambuliaji wa Simba SC, Amisi Tambwe akimtoka beki wa Ashanti United, Hussein Mkongo jioni ya leo (November 06,2013) Taifa.
Ashanti walisawazisha dakika ya 45 mfungaji, Hussein Swedi aliyeunganisha kwa kichwa krosi maridadi ya Hussein Mkongo kutoka wingi ya kulia.

Keshokutwa (Novemba 7 mwaka huu) raundi ya 13 kumaliza mzunguko wa kwanza itakamilika kwa mechi kati ya Yanga na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Azam itakuwa mwenyeji wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Chamazi wakati Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Rhino Rangers na Tanzania Prisons kutoka Mbeya.

Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City, Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons.

MATOKEO:-Jumatano Novemba 6,2013.

JKT Ruvu 1 Coastal Union 0

Ashanti United 2 Simba 4

Kagera Sugar 2 Mgambo Shooting 0

Ruvu Shooting 2 Mtibwa Sugar 2

RATIBA:-Alhamisi Novemba 7,2013.

Azam FC v Mbeya City

Yanga v JKT Oljoro


Rhino Rangers v Tanzania Prisons

MSIMAMO VPL 2013/2014.

NO
TEAMS
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Azam FC
12
7
5
0
20
7
13
26
2
Mbeya City
12
7
5
0
17
8
9
26
3
Young Africans
12
7
4
1
28
11
17
25
4
Simba SC
13
6
6
1
26
13
13
24
5
Kagera Sugar
13
5
5
3
15
10
3
20
6
Mtibwa Sugar
13
5
5
3
19
17
2
20
7
Ruvu Shootings
13
4
5
4
15
15
0
17
8
Coastal Union
13
3
7
3
10
7
3
16
9
JKT Ruvu
13
5
0
8
10
16
-6
15
10
Rhino Rangers
12
2
4
6
9
16
-7
10
11
JKT Oljoro
12
2
4
6
9
16
-7
10
12
Ashanti United
13
2
4
7
12
24
-12
10
13
Tanzania Prisons
12
1
5
6
6
16
-10
8
14
Mgambo JKT
13
1
3
9
3
23
-20
6

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad