Baadhi ya Vifaa vya useremala vilivyotolewa kwa ajili ya Vijana waliohitimu mwaka huu katika chuo cha ufundi Ilemera wilayani Mulena mkoani Kagera.
|
Jumla ya Vijana
22 wa fani ya useremala na ushonaji waliohitimu mwaka huu katika chuo cha ufundi Ilemera wilayani Mulena mkoani kagera
wamepatiwa msaada wa vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi Milioni mbili ili
kuanza maisha ya kujitegemea.
Mkuu wa chuo
hicho Bw Geoffrey Ernest Tilwetwa amebainisha hayo wakati wa mahafali ya tano
ya wahitimu wa fani ya ufundi chuoni hapo na kwamba msaada huo umetolewa na
mfadhili wa chuo mchungaji Olsson Barbro kutoka Sweeden.
Bw Tilwetwa
amesema amesema kuwa wasichana wamepatiwa vyerehani pamoja na vifaa vya ushonaji vyenye thamani ya
shilingi 600,000/= huku wavulana wakipatiwa zana za useremala zenye thamani ya
shilingi 700,000/=.
Aliongeza
kuwa wavulana waliongezewa na fedha
taslimu Tsh.50,000/= kwa ajili ya kujinunulia
mbao ili kutengeneza samani za mfano kwa
wateja.
Ameongeza
kuwa katika kuwafadhili zana hizo uongozi wa chuo na kanisa huwatembelea vijana
kwenye familia zao mara
nne kwa mwaka kujionea maendeleo yao na changamoto zinazowakabili kisha
kutoa ushauri wa kufanikisha maisha yao.
“Pamoja na
juhudi hizo bado chuo hiki tangu kianza mwaka 2002 kinakabiliwa na tatizo la
ukosefu wa umeme kurahisisha ufundishaji wa nadharia na vitendo pamoja na bweni
la wanafunzi”.Alisema.
Hata hivyo
amewaasa vijana hao kutodharau kazi katika maisha yao na kuhakikisha vifaa
walivyopewa vinatunzwa na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa kwa matendo na
kutumia maadili ya kanisa kuwa watumishi bora mbele ya Mungu.
Wakisoma
risala mbele ya baba askofu wa KKKTdayosisis ya kaskazini magharibi mkoani
Kagera mhashamu Elisa Buberwa wahitimu hao licha ya kushukuru walimu wao kwa
mafunzo na kufadhiliwa vitendea kazi wameomba chuo hicho kuondolewa na
changamoto zilizopo.
Wamesema
chuo hicho na wanachuo wanaoendelea kupata fani ya useremala na ushonaji
wanahitaji kupatiwa mavazi ya kikazi (Overall) kwa wavulana ikiwa ni pamoja na bweni
lao,kuongeza matundu ya vyoo ,kuwa na gari la kituo na mlinzi kupatiwa baiskeli ili kutekeleza
vema majukumu yake.
Hata hivyo
Mwenyekiti wa Ilemera Carpentry Centre
for Ophance (ICCO) mchungaji Phinias
Rwakatale wa jimbo la kusini B
ilemera amewahimiza vijana kuwa
na uaminifu katika kazi zao ili waweze kukubalika ndani ya jamii zao.





No comments:
Post a Comment