Mashindano ya Millenium Cup 2013
yaliyoanza mwezi Agost mwaka huu katika kata ya Bugarama wilayani Ngara mkoani
Kagera yamehitimishwa mwishoni mwa wiki (Septemba 29,2013) kwa washiriki
kujinyakulia zawadi mbalimbali.
Mashindano hayo yalijumuisha michezo ya kuvuta
kamba kufukuza kuku kulenga shabaha mpira wa soka na michezo mingineyo kwa
kushirikisha timu za kijiji cha Rwinyana ,Bugarama, Mumiramira,Kihinga na
Bukiriro ambapo aliyefunga mashindano hayo ni
Afisa Tawala wilayani Ngara ,Davidi Mafipa.
Zawadi zilizotolewa ni kwa washindi wa kuvuta kamba Kihinga na Rwinyana kwa kupata elfu 20 kila timu ,
mshindi wa kukimbia na chupa ya maji kichwani na kukalia kiti baada ya kukizunguka Elida Mose maarufu
kwa kuitwa Mama Deusi alipata nguo aina
vitenge viwili na Salome Emanuel kujinyakulia pair ya khanga.
Katika Utoaji wa Zawadi hizo Mshindi wa
tatu katika soka ilikuwa timu ya Rwinyana, Kihinga walikuwa washindi wa pili
huku mshindi wa kwanza na timu yenye nidhamu iliyotoa na mchezaji bora ikiwa ni
Bukiriro FC.





No comments:
Post a Comment