Mkuu wa
wilaya ya Ngara,
Bw Costantine Kanyasu
Akiongea na
wandishi wa
Habari leo
(Octoba 01,2013) ofisini kwake.
|
Serikali
wilayani Ngara mkoani Kagera imekanusha taarifa zilizotolewa katika vyombo vya
habari kuwa kuna Mauaji ya watu wawili yaliyotokea katika kijiji cha Kasulo
wilayani humo, yalitekelezwa kwa shinikizo la viongozi ngazi ya wilaya pamoja
na Mkoa.
Mkuu wa
wilaya ya Ngara, Bw Costantine Kanyasu
ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ,amesema hayo
leo (Octoba 01,2013) ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu taarifa zilizotolewa hivi
karibuni.
Bw. Kanyasu
amesema kuwa mauaji ya watu hao yalitekelezwa na watu 15 wakiongozwa na mmoja
wao anayejiita Mwanaharakati ambaye kwa sasa pamoja na wenzake wanashikiliwa na
Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi za Kisheria.
Amesema kuwa
katika mauaji hayo ni Ng’ombe 17 waliuawa na Wananchi na sio ng’ombe 300 kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya
habari kwa kusikiliza mawazo ya Wananchi bila kuthibitishwa na kamati ya ulinzi
na usalama ya wilaya ya Ngara.
Mkuu wa
wilaya ya Ngara,
Bw Costantine Kanyasu.
|
Katika hatua
nyingine Mkuu huyo wa wilaya ya Ngara ,Mkoani Kagera ametoa wito kwa Wananchi
kuepuka kujichukulia sheria mkononi hasa
kwa kuwaondoa Wahamiaji wanaoishi
Wilayani humo kinyume cha sheria kwani jukumu hilo
linasimamiwa na kikosi maalumu cha Operasheni kimbunga awamu ya pili.





No comments:
Post a Comment