![]() |
Muonekano wa
zawadi za Ngao na fedha tasilimu Laki 7 zilizotolewa kwa Mshindi wa kwanza hadi
wa tatu pamoja na timu yenye nidhamu,mchezaji bora na Mfungaji bora wa BRAYAN CUP 2013.
|
![]() |
Kikosi cha Rusumo FC kikiwa uwanja wa Kokoto mjini Ngara ambapo
kilichuana na Mabingwa wa Wilaya ya Ngara na Kombe la Polisi Jamii Timu ya
Murusagamba FC na kuwafunga kwa bao 1-0.
|
Viongozi wa
Kada mbalimbali na wadau wa Michezo wilayani Ngara mkoani Kagera wametakiwa
kushimakama kwa pamoja ili kuendeleza sekta ya Michezo wilayani humo.
Akihitimisha
mashindano ya kuwania Kombe la Brayan
kwa mwaka huu, Mjumbe wa CCM-NEC Taifa wilaya ya Ngara mkoani Kagera na Mdau mkubwa wa michezo Issa
Samma amesema kuwa kwa kupitia mashindano hayo ya BRAYAN CUP 2013,
yaliyohitimishwa Septemba 29,2013 katika
uwanja wa Kokoto mjini Ngara-hawana budi kujitoa kwa nia ya dhati ili kuleta
maendeleo ya michezo pamoja na vipaji vya wachezaji.
Issa Samma aliwataka
Viongozi na Wadau kujiuliza kwa nini (Why not Me) wanashindwa kuendeleza
michezo mbalimbali wilayani sambamba na kuanzisha Mashindano ili kuleta hamasa
ya Michezo.
Kwa upande
wake Muandaaji wa Kombe hilo la Brayan-Mwl.Godifrey Brayan licha ya kutangaza
kuwa kombe hilo litakuwa likishindaniwa kila mwaka,amewashukuru wadau na
wananchi wa wilaya ya Ngara kwa kuzisaidia timu 12 zilizoshiriki kwa hali na
mali mashindano hayo kwa mwaka huu.
Pia
alishauri Viongozi wa Michezo na Wadau kuacha kuendekeza Majungu na Vikwazo kwa
wadau wanaojitokeza kuendeleza michezo.
Awali
mwenyekiti wa kamati ya mashindano hayo Bahati Kunzi alisema mashindano hayo
yalikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo Kukosekana kwa Waamuzi wa kutosha na
waliofuzu Mafunzo ya Uamuzi,Kutokuwepo kwa Viwanja Bora na Vinavyokidhi Viwango
vya FIFA pamoja na Elimu ndogo ya Uelewa wa masuala ya Mpira wa miguu hususani
kwa Mashabiki jambo ambalo linaweza kuleta vurugu uwanjani.
Katika
fainali hiyo Timu ya Rusumo FC ilifanikiwa kuibuka Bingwa wa kombe hilo kwa
kuwafunga Mabingwa wa Wilaya ya Ngara na Kombe la Polisi Jamii Timu ya
Murusagamba FC kwa bao 1-0 na hivyo kujiondokea na fedha tasilimu shilingi Laki
3 na Ngao.
Mshindi wa
pili Murusagamba FC aliondoka na shilingi Laki 2 na Ngao huku mshindi wa tatu
Walimu FC wakiondoka na Ngao na shilingi Laki Moja.
Timu yenye
nidhamu Rusumo FC iliondoka pia na shilingi Elfu 40,Mfungaji bora Inocent
Buninange kutoka Rusumo FC akiweka shilingi Elfu 30 huku Mchezaji bora Musa
John kutoka Walimu FC na Baraka Nelson kutoka Ngara Starz wakiondoka na
shilingi Elfu 15 kila mmoja.
Timu 12 zilizoshiriki Brayan Cup kwa mwaka huu ni Rusumo FC ,Mtoni FC,Boda boda FC,Benaco FC,Nyakisasa FC,Rulenge white Stars,Mabawe FC,Kabanga FC,Ngara Stars,Walimu FC,Kumubuga FC na Murusagamba FC.
Timu 12 zilizoshiriki Brayan Cup kwa mwaka huu ni Rusumo FC ,Mtoni FC,Boda boda FC,Benaco FC,Nyakisasa FC,Rulenge white Stars,Mabawe FC,Kabanga FC,Ngara Stars,Walimu FC,Kumubuga FC na Murusagamba FC.












No comments:
Post a Comment