JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHITAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARIOPERESHENI KIMBUNGA AWAMU YA PILI YASHIKA KASI KATIKA MIKOA YAKAGERA,
KIGOMA NA GEITA.
Awamu ya Pili ya Operesheni Kimbunga imeweza
kukamata majambazi ya kutumiasilaha 67 na wahamiaji haramu 134 katika kipindi
cha wiki moja tangu kuanzakwake Septemba 21hadi Septemba 27 mwaka huu katika
mikoa ya Kagera, Kigomana Geita.
Silaha zilizokamatwa ni pamoja na bunduki aina
ya SMG Moja, Pisto Moja naMagobole 17 pamoja na risasi 115 zikiwemo za bunduki
aina ya SMG 102 na Risasiza Pisto 13.
Aidha, Magazine mbili zilikamatwa pamoja
na Sare za Jeshi la Burundi.Wahamiaji haramu waliokamatwa wengi wao ni kutoka
nchi za Burundi ambapo raiawake 114 walikamatwa wakiishi nchini kinyume na
sheria wakati raia wa Rwanda 20walikamatwa katika kiindi hicho.
Aidha, watu
Watatu walikamatwa kwa tuhuma za kuhifadhi wahamiaji haramu nchinihuku Lita 271
za gongo , ngozi ya Mbwea, Bangi kilo Tatu na Makokoro 12vilikamatwa wakati wa
operesheni Kimbunga awamu ya Pili ikiwa katika wiki yake yakwanza.
Wakati huo
huo, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera imejipanga kukabiliana na tatizola
wahamiaji haramu ili kuhakikisha kuwa tatizo hilo linafikia mwisho wake na
kuwapanafasi wananchi kufanya shughuli zao za kijamii na kimaendeleo bila ya
hofu yakufanyiwa uhalifu na wahamiaji haramu.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Bi Dari
Rwegasira amewaambia Maafisa Tarafa naWatendaji wa Kata aliokutana nao katika
Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya yaKaragwe, mwishoni mwa wiki iiliyopita kuwa
kuanzia sasa kila kiongozi, kuanziangazi ya Kiijiji/Mtaa, Kata, Tarafa na
Wilaya, atawajibika kwa jinsi anavyoshughulikiakumaliza tatizo la wahamiaji
haramu katika eneo lake.
Wilaya ya Karagwe ni moja ya wilaya zenye tatizo sugu
la wahamiaji haramu ambaowanatuhumiwa kuwanyanyasa wananchi katika baadhi ya
maeneo ya Wilaya hiyo,
kwa
kuendesha vitendo vya wizi wa mifugo, kuvamia maeneo ya kilimo, na pia
kuchochea
uhalifu wa unyang’anyi wa
kutumia silaha na kusababisha mauaji.
Wahamiaji hao haramu wanashutumiwa kufanya
baadhi ya maeneo ya Wilaya yaKaragwe yasipitike kwa urahisi, mojawapo ikiwa ni
eneo la msitu wa Kimisi, ambapoeneo hili limekuwa na matukio mengi ya ujambazi
wa kutumia silaha na wananchikuvamiwa na kuibiwa mali zao na hata wengine
wakipoteza maisha katika matukiohayo.
Maazimio kadhaa yalitolewa katika kikao
hicho kati ya Mkuu wa Wilaya ya Karagwena Watendaji Wakuu wa Wilaya hiyo, ikiwa
ni pamoja na kuwa:
Viongozi kuanzia
ngazi ya Kijiji/Kitongoji, Kata hadi Tarafa kutia saini mkatabawa kushughulikia
wahamiaji haramu, majambazi wa kutumia silaha nawafadhili wao, mifugo haramu
inayoingia nchini kutoka nchi jirani pamoja navitendo vyote vya uhalifu katika
maeneo wanayoyaongoza.
Kiongozi
yoyote wa Kijiji, Kata au Tarafa atakayeshindwa kushughulikiawahamiaji haramu
walioko katika eneo lake atawajibishwa.
Wahamiaji
wote haramu ambao bado wapo katika maeneo mbalimbali yawilaya hiyo wasakwe na
kurejeshwa kwao mara moja.
Msako
uanzishwe mara moja kuwasaka wahamiaji haramu wote ambaowamejificha katika
maeneo ya misitu na ranchi za mifugo zilizoko katika wilayahiyo kwa
kuvishirikisha vyombo vyote vya Utawala na vya Ulinzi na Usalamavilivyoko
katika Wilaya hiyo.
Kila kijiji
kiwe na takwimu sahihi za wageni waliopo katika maeneo yao.
Wahamiaji
haramu wote wanaorejeshwa kwao wasipewe nafasi ya kurudi tenanchini na
mwananchi yoyote atakayebainika kuwapokea au kuwasaidiakurejea atolewe taarifa
haraka ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Vibali vyote
vya Ukazi vilivyotolewa kwa wageni mbalimbali sasa vitakaguliwaupya ili
kuhakiki uhalali wake.
Imeandaliwa
na Timu ya Habari ya Operesheni Kimbunga Septemba30,2013






No comments:
Post a Comment