Timu ya
Manchester City imemaliza rekodi ya Everton kutofungwa katika Ligi Kuu ya Uingereza
baada ya leo hii (Octoba 05,2013) kuifunga mabao 3-1.
![]() |
Contrasting
fortunes: Joe Hart.
|
Vipigo vya
Aston Villa na Bayern Munich viliwafanya City waingie kwa hasira leo na kipa
wao 'kimeo' Joe Hart na kufanya kweli Uwanja wa Etihad Stadium.
Romelu
Lukaku aliifungia Everton bao la kuongoza dakika ya 16, lakini Alvaro Negredo
akasawazisha dakika moja baadaye na Sergio Aguero akafunga la pili kabla ya
mapumziko.
Bao la tatu
la City lilifungwa kufuatia Penati ya kilaini iliyotolewa baada Zabaleta
kusukumwa huku Everton wakinyimwa Penati ya aina hiyo hiyo kufuatia kuangushwa
Lukaku.
Aguero
alipiga Penati hiyo iliyochezwa na Kipa Tim Howard na kugonga mwamba na Mpira
kumbabatiza Kipa huyo na kutinga.
Nao Timu ya Liverpool
wameshika hatamu ya Ligi Kuu Uingereza baada kuifunga Bao 3-1 Crystal Palace
katika Mechi iliyochezwa Anfield.
Bao zote za
Liverpool zilifungwa Kipindi cha Kwanza na Luis Suarez, Daniel Sturride na
Penati ya Steven Gerrard iliyotolewa baada ya Raheem Sterling kuangushwa ndani
ya boksi.
Bao la
Crystal Palace lilifungwa katika Dakika ya 77 na Dwight Gayle.
RATIBA:-BPL:
LIGI KUU ENGLAND 2013/2014.
Jumamosi 5
Oktoba,2013.
Manchester
City 3-1 Everton
Cardiff City
1 -2 Newcastle United
Fulham 1 -0
Stoke City
Hull City 0 -0
Aston Villa
Liverpool 3 -1
Crystal Palace
19:30
Sunderland v Manchester United
Premier League
Table
TeamPPts
Jumapili 6
Oktoba,2013.
15:30
Norwich City v Chelsea
15:30
Southampton v Swansea City
18:00 West
Bromwich Albion v Arsenal
18:00
Tottenham Hotspur v West Ham United








No comments:
Post a Comment