Matokeo
hayo, yanaifanya Simba SC
itimize pointi 15 baada ya mechi saba
na kuendelea
kushikilia usukani wa Ligi Kuu.
|
Ligi Kuu Soka
ya Vodacom Tanzania Bara imeendelea leo(Octoba 05,2013) huku vinara Simba SC
wakipunguzwa kasi kwa sare ya bao 1-1 na Ruvu Shooting katika Uwanja wa Taifa, Mjini Dar es Salaam na
Azam FC pia wakitoka sare ya bila kufungana na Coastal Union Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga.
Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam, Simba SC ililazimika kusubiri hadi dakika ya 51 kupata
bao la kusawazisha kwa penalti kupitia kwa Amisi Tambwe, kufuatia Betram
Mombeki kuangushwa kwenye eneo la hatari, baada ya Ruvu Shooting kutangulia
kufunga dakika ya nane kupitia kwa Said Dilunga.
Hata hivyo,
wachezaji wa Ruvu Shooting walimzonga refa Mohamed Theophil wakipinga penalti
hiyo, kabla ya kulainika na kukubali ipigwe- na Mrundi Tambwe akaenda kufunga
bao lake la Nane ndani ya mechi saba katika msimu wake wa kwanza Simba SC.
Matokeo
hayo, yanaifanya Simba SC itimize pointi 15 baada ya mechi saba na kuendelea
kushikilia usukani wa Ligi Kuu.
Baadhi ya
wachezaji wa Coastal Union.
|
Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga mechi ilikuwa kali, ilitawaliwa na vurugu za mashabiki tangu
hata kabla mchezo haujaanza na matokeo kumalizika kwa sare ya bao 0 - 0.
Baada ya
kucheza na Azam FC siku ya jumamosi
Octoba 05), Wagosi wa Kaya watakuwa wamebakisha mechi sita kukamilisha
mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ambazo ni dhidi ya Ashanti United Octoba 13 siku
ya Jumapili katika uwanja wa Chamazi
jijini Dar es Salaam.
Mechi
nyingine ni dhidi ya Kagera Sugar (J2 Oct 19, Bukoba), Simba SC (J5 Oct 23,
Tanga), Mtibwa Sugar (J1 Oct 26, Tanga), Mgambo JKT (J5 Oct 30, Tanga), mwisho
watamalizia mzunguko wa kwanza katika Mkoa wa Pwani wakicheza dhidi ya JKT Ruvu
Jumamosi Novemba 2.
Kikosi cha
Timu ya Mbeya City wakiwa katika picha ya Pamoja katika uwanja wa Sheikh Amri
Abeid mjini Arusha…na Goli la kwanza Lililo Fungwa na Expedito Kiduko dakika ya
35 ya mchezo huo.
|
MATOKEO /RATIBA
LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA
2013/2014.
Jumamosi Oktoba 05,2013.
Ruvu
Shootings 1-1 Simba SC
JKT Ruvu 2-0
Kagera Sugar
Coastal
Union 0-0 Azam FC
JKT Oljoro
1-2 Mbeya City
VPL-MSIMAMO
2013/2014.
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GD
|
GF
|
POINTI
|
1
|
Simba SC
|
7
|
4
|
3
|
0
|
11
|
16
|
15
|
2
|
JKT Ruvu
|
7
|
4
|
0
|
3
|
4
|
8
|
12
|
3
|
Azam FC
|
7
|
2
|
5
|
0
|
3
|
9
|
11
|
4
|
Coastal Union
|
7
|
2
|
5
|
0
|
3
|
6
|
11
|
5
|
Mbeya City
|
7
|
2
|
5
|
0
|
2
|
8
|
11
|
6
|
Kagera Sugar
|
7
|
3
|
2
|
2
|
2
|
7
|
11
|
7
|
Ruvu Shooting
|
7
|
3
|
1
|
3
|
2
|
7
|
10
|
8
|
Yanga SC
|
6
|
2
|
3
|
1
|
4
|
11
|
9
|
9
|
Rhino Rangers
|
7
|
1
|
4
|
2
|
-1
|
7
|
7
|
10
|
Mtibwa Sugar
|
6
|
1
|
4
|
1
|
-1
|
5
|
7
|
11
|
JKT Oljoro
|
7
|
1
|
2
|
4
|
-3
|
4
|
5
|
12
|
Mgambo JKT
|
6
|
1
|
2
|
3
|
-8
|
2
|
5
|
13
|
Prisons FC
|
6
|
0
|
4
|
2
|
-6
|
3
|
4
|
14
|
Ashanti United
|
7
|
0
|
2
|
5
|
-11
|
4
|
2
|
Jumapili (Octoba 06,2013) Mabingwa watetezi Yanga watakuwa Nyumbani Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza na Mtibwa Sugar.
Jumapili
Oktoba 6,2013.
Yanga v
Mtibwa Sugar
Mgambo JKT v
Tanzania Prisons





No comments:
Post a Comment