Serikali imewataka wasimamizi watakaosimamia mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi kufanya
kazi yao ya kusimamia kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu, huku ikiwaonya
wale watakaokiuka agizo hilo kuwa watachukulia hatua za kisheria.
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo
Mulugo ametoa wito huo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jana (Septemba 09,2013) jijini Dar es Salaam
kuhusu mtihani huo, ambao unaotarajiwa kufanyika Septemba 11 na 12 mwaka huu.
"Napenda
kuwaasa tena wasimamizi kujiepusha na vitendo hivyo vya udanganyifu kwani
Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote
atakayebainika kukiuka taratibu za mitihani" alisema Mulugo.
Naibu Waziri
huyo alisema kuwa wapo baadhi ya wasimamizi ambao wamekuwa nawakishriki katika
kuwasadia watahiniwa kufanya udanganyifu kwenye mitihani yao.
Katika
mtihani huo Jumla ya watahiniwa 868,030 wamesajiliwa kufanya mtihani huo, kati
yao wavulana 412,105 sawa na asilimia 47.47 na wasichana 455,925 sawa na
asilimia 52.52.
![]() |
| Philipo Mulugo. |
Naibu Waziri
huyo aliendelea kusema kuwa kuna jumla ya watahiniwa 844,810 ambao wanatarajiwa
kufanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili kati yao wavulana 400,335 na
wasichana 444,475.
Wanafunzi 22,535 kati yao wavulana ni 11,430 na wasichana ni
11,105 watafanya mthani huo kwa lugha ya Kiingereza ambao ndio waliyokuwa
wakiitumia kujifunzia.
Kwa upande
wa watahiniwa wasioona, waliosajiliwa kufanya mtihani huo ni 88 wakiwemo
wavulana 56 na wasichana 32. Watahiniwa wenye uoni hafifu ambao huhitaji
maandishi makubwa ni 597.
Wanaotarajiwa kufanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili
ni watahiniwa 546 kati yao wavulana ni 263 na wasichana ni 283. Wanaotarajiwa
kufanya mtihani kwa lugha ya Kiingereza ni watahiniwa 51 kati yao wavulana ni
21 na wasichana 30.
Aidha,
Mulugo alisema kuwa maandalizi yote kwa ajili nya mtihani huo yamekamilika
ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa karatasi za mtihani, kusambazwa kwa fomu
maalum (Optical Mark Reader, (OMR) za kujibia mtihani na nyaraka zote muhimu
zinazohusika.
Akijibu
swali lililoulizwa na waandishi wa habari katika mkutano huo juu ya watahiniwa
kutumia fomu za OMR kujibia mtihani Naibu Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani
Tanzania Dkt. Charles Msonde alisema kuwa wanafunzi wameandaliwa vizuri kutumia
fomu hizo na zimeonesha mafanikio makubwa.
Dkt. Msonde
alisema katika kipindi cha mwaka 2012 fomu zote zilizotumika kujibia mtihani
huo zilipita vizuri kwenye kompyuta na ambazo ziligoma kutokana na sababu
mbalimbali zilisafishwa na kunyooshwa na hatimaye kukamilika na kusahihishwa.
Masomo
yatakayotahiniwa katika mtihani huo ni Kiswahili, Kiingereza, Sayansi ,Hisabati
na maarifa ya jamii.







No comments:
Post a Comment