Serikali ya Tanzania imesema Raia wanaoishi nchini Kinyume cha Sheria ,walioolewa na Watanzania wanaruhusiwa kubaki nchini,
hawalazimiki kuvunja ndoa zao ingawa wanatakiwa kupata kibali maalumu kutoka
Idara ya Uhamiaji.
Akizungumza
mjini Bukoba jana (Septemba 09,2013), Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, alisema
wahamiaji hao walioolewa wanatakiwa kwenda Idara ya Uhamiaji kupata hati
hizo.
“Hatupendi
kuachanisha familia zilizoishi kwa zaidi ya miaka miwili mfululizo, wanatakiwa
kwenda uhamiaji kuhalalishwa na baadaye ikigundulika hana tatizo anaweza kupewa
uraia,” alisema Kanali Massawe.
Pia, alisema
kwa mujibu wa sheria, mhusika atapewa kibali alichokiita ‘Independence Pass’
kitakachomwezesha kuendelea kuishi
nchini na kwamba, kinyume chake itakuwa ni kuvunja haki za binadamu.
![]() |
| Kanali Mstaafu Fabian Massawe. |
Akizungumzia
zoezi la kurudisha Raia wanaoishi Nchini kinyume che Sheria na utaratibu wa Idara ya Uhamiaji lililoanza rasmi Septemba 6, mikoa ya
Kagera, Geita na Kigoma, Mkuu Msaidizi wa Operesheni hiyo, Simon Sirro, alisema
tayari wamewakamata 1,851.
Pia, Sirro
alisema ng’ombe 1,765, sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na bunduki
saba vimekamatwa na kwamba,
wahamiaji wanaokamatwa wanarudishwa kwa
mujibu wa sheria kwa kuzingatia haki za binadamu.
Na Phinias
Bashaya:- Mwananchi.







No comments:
Post a Comment