Timu hizo zikimenyana katika uwanja wa wilaya ya Ngara wa Kokoto ambao hauna kiwango kizuri cha kuchezewa mechi ambapo Murusagamba FC wamefanikiwa kutinga Fainali ya kuwania Brayan Cup.
|
Muonekano wa Mashabiki wakifatilia mchezo kati ya Timu ya Murusagamba FC waliposhuka kumenyana na Timu ya Kabanga FC na Murusagamba FC kuitwanga Kabanga FC mabao 2-1.
|
Bi.Niniani Bakari mratibu wa soka la Wanawake wilayani Ngara mkoani Kagera na pia Diwani wa Viti Maalumu tarafa ya Kanazi ,ambaye leo alishuhudia timu yake ya Ngara ikifungwa bao 1-0 na Runazi .
|
Afisa
Michezo wa wilayani Biharamulo mwenye
kofia Dioniz Magezi akiwa na Mwl Adolf Gisuka wakiwa na mchezaji wa soka la
kike leo(Septemba 08,2013) kwenye uwanja
wa Posta ya zamani ,Mjini Ngara.
|
Mashindano
ya kuwania Kombe la Brayan au BRAYAN CUP 2013 ,inayoshirikisha timu toka wilayani Ngara mkoani Kagera na Ijumaa ,Jumamosi(Septemba 07,2013) na
Jumapili (Septemba 08,2013) michezo ya hatua ya Robo fainali ilichezwa katika
Uwanja wa Kokoto Mjini Ngara.
Siku ya Ijumaa(Septemba 05,2013) Timu ya
Walimu FC ilifanikiwa kuingia hatua ya Mwisho ya Fainali kwa kuwaondosha Rulenge White Stars kwa kuwafunga magoli 2-1
kwa magoli ya Mwl.Severin John na Moses John.
Jumamosi(Septemba
07,2013) Ngara Stars wakaondoshwa na Vijana wa Boda-Rusumo FC kwa kuzabwa bao
1-0 katika mchezo ulienda dakika 120 baada ya dakika 90 timu hizo kutoshana
nguvu ya bila kufungana.
Leo Jumapili
(Septemba 08.2013) Mabingwa wa soka wa wilaya Murusagamba FC wameshuka katika
uwanja huo wa Kokoto kumenyana na Timu ya Kabanga FC na Katika mchezo huo ,timu ya Murusagamba
FC imetinga hatua ya Fainali ya Brayan Cup kwa kuitwanga Kabanga FC mabao 2-1,
yaliyofungwa na Gilbaert Gozibert na
Egason Fredrick huku Kabanga FC bao lao
la kufutia machozi likifungwa na Yasiri
Jumanne.
Kombe hilo
sasa limemaliza michezo ya hatua ya Robo Fainali na timu zilizofanikiwa kusonga
mbele ni Walimu FC,Rusumo FC na Murusagamba FC ambao kwa mujibu wa kanuni timu
hizo zitacheza mtindo wa Ligi(Pointi) ili kumpata Bingwa wa Brayan Cup 2013
ambaye mshindi wa kwanza ataondoka na zawadi ya shilingi 300,000.





No comments:
Post a Comment