Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) inaingia raundi yake ya tano kesho (Septemba 21 mwaka huu) kwa
mechi huku vinara Simba wakiwakaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting Stars na
Rhino Rangers ya Tabora.
Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons katika
pambano litakalochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Nayo Kagera
Sugar itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake wa Kaitaba mjini Bukoba kuvaana na
Ashanti United ya Dar es Salaam katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob
Adongo kutoka Mara.
Ligi hiyo
itakamilisha mzunguko wa tano keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) kwa mechi tatu
ambapo Azam na Yanga zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku JKT Ruvu
ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Ruvu
Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa mgeni wa
Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga.
Wakati huo
huo, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea wikiendi hii kwa mechi kumi na
moja. Kundi A kesho (Septemba 21 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Transit
Camp na Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam), Tessema na African
Lyon (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi).
Ndanda
itacheza na Villa Squad kwenye Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati keshokutwa
(Septembe 22 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Polisi Dar es Salaam na
Friends Rangers katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi B
kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Mkamba Rangers dhidi ya Burkina Faso kwenye
Uwanja wa CCM Mkamba, na Mlale JKT itakuwa mwenyeji wa Kurugenzi Mafinga kwenye
Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) ni Majimaji
na Kimondo katika Uwanja wa Majimaji.
Mechi za
kundi C kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Pamba dhidi ya Polisi Dodoma (Uwanja
wa CCM Kirumba, Mwanza), Stand United na Polisi Tabora (Uwanja wa Kambarage,
Shinyanga) na Kanembwa JKT itacheza na Mwadui kwenye Uwanja wa Kawawa ulioko
Ujiji.
Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) Polisi Mara na Toto Africans
zitacheza Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
Boniface
Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


.jpg)



No comments:
Post a Comment