 |
Wanafunzi wapatao 107 kutoka shule za Msingi za Buhororo,Rulenge,Munjebwe
na Mayenzi wilayani Ngara Mkoani Kagera wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa
Mashindano ya Bonanza la siku moja la Michezo mbalimbali Ngazi ya wilaya ya
Ngara lililoandaliwa na Idara ya Elimu shule za Msingi kwa ufadhili wa shirika la Jambo Bukoba na kufanyika
Septemba 20,2013 katika viwanja vya shule ya Msingi Buhororo.
|
 |
Bonaza hilo
lilifunguliwa na Kufungwa na Afisa Elimu Idara ya Msingi wilayani Ngara
Bw.Simon Mumbee ambapo pamoja na mambo mengine alikabidhiwa zawadi ya Mpira
wenye Maandishi ya Mdhamini wa Jambo Bukoba (Bayern Munich) na Ms.Sandra Kagerer kutoka Ujerumani kwa Niaba ya Jambo Bukoba mkoa wa Kagera.
|
 |
Afisa Elimu Idara ya Msingi wilayani Ngara
Bw.Simon Mumbee akionesha zawadi ya Mpira aliyokabidhiwa na Jambo Bukoba mkoa wa Kagera na pembeni yake ni Afisa Michezo wilaya ya Ngara Saidi Salumu(track suit ya blue) na Mratibu Elimu Kata ya Kibimba.
|
 |
| Baadhi ya wanafunzi wa shule za Msingi za Buhororo,Rulenge,Munjebwe
na Mayenzi wilayani Ngara Mkoani Kagera wakiendelea na michezo ya kuunda maumbo ya aina mbalimbali kwa kutumia kamba wakati wa
Mashindano ya Bonanza la siku moja la Michezo mbalimbali Ngazi ya wilaya ya
Ngara lililoandaliwa kwa ufadhili wa shirika la Jambo Bukoba na kufanyika
Septemba 20,2013 katika viwanja vya shule ya Msingi Buhororo. |
 |
| Afisa Elimu Idara ya
Msingi wilayani Ngara
Bw.Simon Mumbee akifungua Bonanza hilo la Jambo Bukoba kwa kuwataka washiriki kushiriki kwa ushindani pamoja na kulishukuru shirika la Jambo Bukoba kwa Kutoa Elimu na Kuibua vipaji pamoja na Kuviendeleza kupitia michezo kwa shule za msingi huku pembeni yake ni Mratibu wa Michezo toka Shirika la Jambo Bukoba mkoa wa Kagera Bw.Gonzaga Steven na Afisa Michezo wilaya ya Ngara Saidi
Salumu. |
 |
Muonekano wa Wanafunzi wa
shule ya msingi Buhororo wilayani Ngara mkoani Kagera wakiwa katika mashindano
ya Bonanza dhidi ya wenzao kutoka Shule za Msingi Rulenge ,Munjebwe na Mayenzi wilayani humo
,Bonanza hilio liliandaliwa na Idara ya Elimu shule za Msingi kwa ufadhili wa Shirika la Jambo Bukoba.
|
 |
Wanafunzi wapatao 107 kutoka shule za Msingi za Buhororo,Rulenge,Munjebwe
na Mayenzi wilayani Ngara Mkoani Kagera wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa
Mashindano ya Bonanza la siku moja la Michezo mbalimbali Ngazi ya wilaya ya
Ngara lililoandaliwa kwa ufadhili wa shirika la Jambo Bukoba na kufanyika
Septemba 20,2013 katika viwanja vya shule ya Msingi Buhororo.
|
Bonanza hilo kwa Mujibu wa Afisa Elimu Idara
ya Msingi wilayani Ngara Bw.Simon Mumbee amebainisha kuwa ni muendelezo wa
michezo ambayoimekuwa ikifanyika toka mwaka jana ambapo kwa wilaya ya Ngara Mkoani
Kagera timu 4 zilishiriki na kutoa Bingwa wake shule ya Msingi Rulenge ambayo ilienda
kushiriki Bonanza la Jambo Bukoba ngazi ya Mkoa wa Kagera.
Michezo
iliyochezwa ni pamoja na Kunyang’anyana mpira,Mchezo wa Aljebra,Mchezo wa
partner football na Ten Pass.
Aidha Mratibu
wa Michezo toka Shirika la Jambo Bukoba mkoa wa Kagera Bw.Gonzaga Steven
amesema Bingwa wa Bonanza hilo atakayepatikana ataiwakilisha Wilaya ya Ngara
katika Bonanza kama hilo Ngazi ya Mkoa wa Kagera hapo Mwakani.
No comments:
Post a Comment