![]() |
| Amisi Tambwe wa Simba SC dk za 29 na 33. |
Pamoja na
matokeo hayo, Simba SC bado inaongoza Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 11 baada ya
kucheza mechi tano, wakati Mbeya City inafikisha pointi saba baada ya mechi
tano pia.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Abdallah Kambuzi wa Shinyanga, Charles
Mbilinyi na Juma Mwita wa Mwanza, hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa
mbele kwa mabao 2-1.
Mshambuliaji
wa Simba SC, Amisi Tambwe akimtoka beki wa Mbeya City Anthony Matogolo katika
mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo. Timu hizo zilitoka
2-2.
Simba SC
inayofundishwa na mshambuliaji wake wa zamani, Abdallah Athumani Seif ‘King
Kibaden’, ilipata mabao yake yote kupitia kwa Amisi Tambwe aliyefunga katika
dakika za 29 na 33.
Mbeya City,
timu ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya inayofundishwa na Juma Mwambusi, bao la la
kipindi cha kwanza lilifungwa na Paul Nonga dakika ya 37, wakati la kusawazisha
lilifungwa na Richard Peter dakika ya 69.
Tambwe
alifunga bao lake la kwanza akiunganisha krosi ya Chanongo, wakati la pili
ilikuwa pasi ya Betram Mombeki.
Paul Nonga
alifunga bao lake kwa shuti kali ambalo lilimshinda kipa wa Simba SC, Abbel
Dhaira Peter alifunga bao lake akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na
Mwagane Peter.
Katika mechi
nyingine, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wenyeji Mgambo Shooting Stars walitoka
sare ya 1-1 na Rhino Rangers ya Tabora, Prisons ilitoka 1-1 na Mtibwa Sugar
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya, wakati Kagera Sugar ilishinda 3-0
dhidi ya Ashanti United ya Dar es Salaam Uwanja wa Kaitaba.
Ligi hiyo
itakamilisha mzunguko wake wa tano kesho(Septemba 22,2013) kwa mechi tatu moja
ndiyo hiyo ya Azam na Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku JKT Ruvu
ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Ruvu
Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa mgeni wa
Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga.






No comments:
Post a Comment