![]() |
Mwenyekiti
wa Chadema Mh Freeman Mbowe akihutubia katika mkutano uliojumuisha Vyama vya
Siasa, Wanaharakati na taasisi za Dini kujadili Suala la Mchakato wa Katiba
unaoendelea :-Septemba 21,2013.
|
![]() |
Mwenyekiti
wa NCCR Mageuzi Mh James Mbatia akihutubia wakazi wa Dar es salaam katika
Mkutano wa suala la katiba uliofanyika katika viwanja vya Jangwani.
|
![]() |
Mwanasheria wa Chadema Mh Mabere Marando akihutubia mamia ya
wakazi wa Dar es salaam Katika Mkutano wa Katiba.
|
![]() |
Mnadhimu
mkuu wa Kambi ya Upinzani na mbunge wa Iramba Mh Tundu Lissu akihutubia katika
mkutano wa Katiba katika Viwanja vya Jangwani Dar es salaam.
|
![]() |
Mbunge wa
Ubungo Mh John Mnyika akihutubia katika Mkutano wa Katiba Ulioitishwa na Umoja
wa Vyama vya siasa, Wanaharakati na Viongozi wa Dini.
|
![]() |
Mchungaji
Zakaria Kakobe akihutubia katika Mkutano wa Katiba Viwanja vya Jangwani.
|
![]() |
Mhadhiri wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Azaveli Lwaitama.
|
![]() |
Mamia ya
wakazi wa Dar es Salaam wakisikiliza Viongozi wa Vyama Vya Siasa katika mkutano
wa Suala la Katiba uliofanyika katika Viwanja vya Jangwani.
|
![]() |
Mamia ya
wakazi wa Dar es Salaam wakisikiliza Viongozi wa Vyama Vya Siasa katika mkutano
wa Suala la Katiba uliofanyika katika Viwanja vya Jangwani.
|
Vyama vya
upinzani jana vilifanya mkutano mkubwa kuwashawishi wananchi kupinga kile
walichokiita kuhujumiwa kwa mchakato wa Katiba Mpya, wakitangaza Oktoba 10 kuwa
siku ya Watanzania wote kushiriki katika maandamano kushinikiza wapewe haki ya
kuandaa Katiba yao.
Wakizungumza
kwa kupokezana katika Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam jana ( Septemba 21,2013) ,
wenyeviti wa vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF, walieleza kuwa wataendelea
kushirikisha taasisi za kiraia kupinga hujuma dhidi ya mchakato wa Katiba Mpya
na kwamba hawatakubali endapo Rais Jakaya Kikwete atasaini Muswada wa
Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba Mpya.
Akizungmza
katika mkutano huo Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba alisema chama chake
hakitakubali endapo Rais Kikwete atasaini muswada huo kwa kuwa una lengo la
kupata Katiba Mpya isiyokuwa na tija kwa taifa.
Alisema kuwa Katiba inayoandaliwa
ni kwa ajili ya Watanzania wote na siyo kundi la watu, hasa CCM na kwamba
mchakato wa kuwapata wajumbe 166 wa Bunge la Katiba kutoka makundi mbalimbali
siyo sahihi.
“Haiwezekani
kila taasisi ikateuwa wajumbe tisa ambao majina yao yatakwenda kuchakachuliwa
na usalama wa taifa, kisha kupata majina ya watu wanaowataka wao, kitu hiki
kama CUF hatutakubali,” alisema Profesa Lipumba na kuongeza:-
“Hatutarudi
nyuma na kukubali kuendelea na mchakato huu endapo Rais atasaini muswada huu.
Tutaendeleza harakati za kupinga kwani bila hivyo tutapata Katiba Mpya
isiyokuwa na tija.”
Kwa upande
wake, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema kuwa ni wakati wa kukaa
meza moja ya mazungumzo kuondoa tofauti zilizopo ili kulinusuru taifa kuingia
katika machafuko.
Alisema kama
taifa, linatakiwa kujifunza kutoka mataifa mengine yalivyotokea maafa katika
michakato ya kuandikwa kwa Katiba Mpya.
“Ni wakati
wa kukaa meza moja, kwa kushirikisha wadau mbalimbali kwani Katiba inayotafutwa
ni ya Watanzania wote na siyo ya CCM,” alisema Mbatia na kuongeza:-
“Lazima
tupate Katiba Mpya kwa gharama yoyote ile, iwe ndani au nje ya Bunge ili
kuhakikisha tunapata Katiba ya Watanzania wote.”
Mwenyekiti
wa Chadema Freeman Mbowe alisema kosa kubwa katika kudai haki ni woga na hatutapata
Katiba Mpya kama tutaendelea kuwa taifa la watu wenye hofu.
Tunataka kukutana
na makundi mbalimbali katika jamii ambayo ni viongozi wa dini, wasomi na watu
wa makundi mengine kuwaeleza kinachoendelea sasa hivi.
Hata
migogoro ya kiimani baina ya Wakristo iliyotokea nchini imesababishwa na katiba
iliyopo sasa, kama Rais atasaini wao hawatashiriki Bunge la Katiba na watatumia
kila mbinu iliyopo duniani kuueleza umma nini kimetokea na hawataendelea
kunyenyekea vitisho vya Jeshi la Polisi.
Tunalaani
mchakato wa katiba kuhodhiwa na chama kimoja na tunatangaza Oktoba 10, mwaka
huu kuwa ni siku maalumu ya kudai katiba na sasa hawataenda tena Ikulu kwani
inaaminika huko ni kwenda kunywa chai na watatangaza maandamano nchi nzima.
“Tumemwambia
IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema) kuwa hatutaomba
ruhusa bali tutampa taarifa.
Tunaomba walio makanisani na misikitini kutafuta
katiba mpya na jambo la mwisho Jumatato tutaenda kufanya mkutano kama huo
Zanzibar,” alisema Mbowe.
Mwenyekiti
wa Chama cha NLD, Dk Emmanuel Makaidi alisema chama chake kinapinga namna
mchakato wa Katiba ulivyoendeshwa kwasababu kilichopelekwa bungeni kilikuwa
Muswada wa Katiba Mpya, lakini kilichopo mitaani ni Mchakato wa Rasimu ya
Katiba Mpya.
“Tunawaambia
CCM hawatengenezi Katiba Mpya, wanachofanya ni danganya toto kwa kuwa
wanatakiwa kuirudisha Katiba ile ile ya awali.
Naye Askofu
Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe
aliyefika katika viwanja hivyo alisema kuwa Rais Kikwete akisaini muswada huo,
Watanzania watajua kuwa hana nia njema na taifa kwa kuwa wengi wanaipinga.
“Mimi natega
masikio kusikia kama utasaini au la ili kujua kama unawatega na kuwahadaa
Watanzania. Tunakuomba usikubali mtego huo,” alisema Kakobe akimwambia Rais
Kikwete.
Alisema
tangu awali CCM ilikuwa ikipinga kuandaliwa kwa Katiba Mpya, ingawa Rais Jakaya
Kiwete alijitosa na kukubali mchakato huo kuanza nchini.
“CCM
ilikataa katakata Katiba isianzishwe. Jakaya Kikwete pekee yake alijipiga kifua
akakubali ingawa alishambuliwa kuwa amefanya makosa,” alisema Kakobe.
Mhadhiri
mstaafu wa Chuo Kukuu cha Dar es Salaam(Udsm), Dk Azaveli Lwaitama alisema kuwa
duniani kote shinikizo la kuundwa kwa Katiba Mpya hutoka nje ya Bunge na
Serikali iliyopo madarakani.
“Tangu mwaka
1992 vyama vya upinzani vilikuwa vikitaka Katiba Mpya... Katiba Mpya huzaliwa
na wanamapinduzi waliopo nje ya Bunge,” alisema Dk Lwaitama.
Akizungumzia
ushirikiano wa vyama kumzuia Rais asisaini Sheria ya Rasimu ya Katiba, alisema:
“ Ukifanya jeuri kwa sababu upo madarakani, watu uliodhani wamegombana
watashirikiana.”
Mbunge wa
Ubungo John Mnyika, alisema Mahakama ya wananchi ndiyo itakayotoa uamuzi wa
mwisho.
“Ninyi ndiyo
Mahakama yenye uamuzi wa mwisho, tunasubiri mwongozo wenu, mtakachosema
tutafanya,” alisema Mnyika.
Kabla
kuwasili kwa viongozi wakuu wa vyama hivyo vya siasa kwenye Viwanja vya
Jangwani, jana wafuasi wao walikuwa kwenye makundi wakichambua baadhi ya mambo
yaliyoonekana kuleta utata kwenye mchakato wa Katiba Mpya.
Rangi za
bluu, nyekundu na nyeupe zinazotumiwa na vyama vilivyoshiriki kumtaka Rais
Jakaya Kikwete kutosaini Muswada wa Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba Mpya
zilionekana kuzagaa katika viwanja hivyo.
Magari ya
Polisi yalionekana kuzunguka maeneo ya viwanja hivyo kuhakikisha ulinzi unaimarika
wakati wote wa mkutano.
Nao wafuasi
wa vyama hivyo waliokuwa wamevaa suti nyeusi, miwani na mashati meupe
waliimarisha ulinzi katika eneo la mkutano, wengine wakiingia Viwanja vya
Jangwani kutoka eneo la Barabara ya Morogoro, huku wakibeba mabango, bendera za
vyama hivyo na picha za viongozi wao wakiimba nyimbo mbalimbali.
Wengi wa
wafuasi hao walifika uwanjani hapo kwa kuletwa na mabasi madogo aina ya Coaster
na wengine wakija kwa makundi kutokana Jeshi la Polisi kuzuia kufanyika kwa
maandamano.















No comments:
Post a Comment