Mawaziri
watatu kutoka Tanzania Rwanda na Burundi wametiliana saini ya kuanza kutekeleza
mradi wa uzalishaji umeme ulioko katika maporomoko ya Rusumo mpakani mwa
Tanzania na Rwanda.
Waziri wa
nishati na madini wa Tanzania Profesa Sospita Muhongo amesema hayo septemba
12,mwaka huu katika mkutano wa sita wa wataalamu wa mradi
huo na mawaziri wa nchi zao uliofanyika
katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Profesa
Muhongo amesema kuwa wataalamu wa mradi
huo pamoja na wafadhili wa
wamejadiliana na kufikia makubaliano ya kuanza kuujenga mwaka 2015 na
kuukamilisha mwaka 2018 kwani ulioanza kufanyiwa utafiti tangu mwaka 1974.
Aidha
Profesa Muhongo amesema katika ujenzi wa mradi huo wa megawati 80
kila nchi itapata megawati 27 na
mradi huo kila nchi itakuwa na usimamizi wa 30% ambapo asilimia nyinginezo
zitawekezwa katika mto Nile.
Katika Hatua
nyingine Profesa Muhongo amesema kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB)
imekubali kutoa shilingi milioni 870 kwa ajili ya kupeleka umeme kutoka mjini
Ngara hadi Rusumo kwa wananchi na taasisi zake.
Ameongeza
kuwa watendaji wa shirika la umeme
nchini TANESCO kanda ya ziwa hawana budi kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha wanatoa huduma kwa wananchi
kwa kuwapatia nishati ya umeme kwa wakati.
“Watendaji
wa wizara yangu watumie uzalendo katika kutekeleza masuala ya kitaifa
katika mradi huu kwa kuboresha maisha
ya wananchi kuliko kuhudhuria mikutano
na kutelekeza maazimio wanayokubaliana”.
Akiongeza kuwa “Serikali imedhamilia kusambaza umeme katika maeneo ya vijijini katika halmashauri za wilaya kwa 30%
ifikapo mwaka 2015 ambapo na bajeti ya wizara yangu mwaka huu imeongezeka kutoka Bil 642
hadi Tilioni 1.4”.Alisema Muhongo.
Hata hivyo
waziri wa nishati na madini wa Tanzania Profesa Sospita Muhongo ametoa rai kwa
wazabuni ,wakandarasi na wataalamuwa mradi huo
kutumia uzalendo kwa kuepuka
mianya ya Rushwa na kuujenga chini ya viwango na kwamba atawachukulia hatua
watakaofanya ubadhilifu.
Kwa upande
wake waziri wa miundombinu wa nchini Rwanda profesa Silas Rwakabamba amewashauri wananchi wa nchi tatu zenye mradi huo kutumia fursa zitakazojitokeza katika mradi
wa uzalishaji umeme wa rusumo ili kuinua maisha yao kiuchumi.
Profesa Rwakabamba amesema umeme huo utanufaisha
wananchi zaidi ya nchi tatu zilizolengwa
kwa kujumuisha upatikanaji wa nafasi za ajira na kukuza kipato cha kiuchumi
katika sekta mbalimbali.
Amesema
katika utoaji wa ajira kwa wataalamu wa mradi huo mawaziri wamekubaliana kuhakikisha zinatolewa
fursa kwa nchi zote husika ili
kuhakikisha manufaa yanapatikana bila
kuwepo upendeleo wala hujuma yoyote.
Picha/Habari
Na: Shaaban Ndyamukama.








No comments:
Post a Comment