Villarreal v/s Real Madrid 2 -2 : Bale akifunga bao lake la kwanza kwa Real Madrid. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 15, 2013

Villarreal v/s Real Madrid 2 -2 : Bale akifunga bao lake la kwanza kwa Real Madrid.

Mabao 203 katika mechi 203 kwa Cristiano Ronaldo; moja katika mchezo mmoja kwa Gareth Bale. 
Hiyo ndiyo ilikuwa mwanzo wa faida za kutoa Euro Milioni 100 kumsajili mchezaji huyo baada ya Bale kufunga bao lake la kwanza Real Madrid jana (Septemba 14,2013) usiku katika sare ya 2-2 dhidi ya Villarreal.




Bale alifunga kipindi cha kwanza na Ronaldo akafunga kipindi cha pili katika mchezo huo wa La Liga.

The three players who could define a generation in Madrid, Isco (left), Ronaldo and Bale.

Carlo Ancelotti hasn't had the best of starts as Real Madrid coach, with many of his players new.


Yellow submarine: It certainly wasn't all plain-sailing as Villarreal scored the opening goal through Cani.

Old Spurs boy: Giovani Dos Santos (centre) used to play Bale at Tottenham


Septemba 14,2013 Usiku, Katika LA LIGA:- Klabu ya Real Madrid  ikimchezesha  rasmi mchezaji wa bei kubwa Duniani, Gareth Bale, ambae alifunga Bao moja na Supastaa mwenzake Cristiano Ronaldo kufunga Bao jingine wakati Real Madrid wakibanwa na kutoka Sare ya Bao 2-2 walipocheza Ugenini na Villareal huku Cani akiipa Bao la kwanza Villareal na la kusawazisha kwa Bao la Dos Santos.

Mabingwa Watetezi FC Barcelona waliichapa Sevilla Bao 3-2 hapo Jana Pia  kwenye Mechi ya La Liga na  kwa bao za  kufungwa na Alves, Lionel Messi na Sanchez wakati Bao za Sevilla zilifungwa na Rakitic na Coke.

SERIE A: - Uwanjani San Siro hapo Jana (Septemba 14,2013), Inter Milan na Juventus zilitoka Sare ya Bao 1-1 katika Mechi  iliyobatizwa Derby D’Italy.
Inter Milan  walitangulia kufunga katika Dakika ya 73 kwa Bao la Mauro Icardi na Juventus  kurudisha Dakika 2 baadae kwa Bao la Arturo Vidal.

BUNDESLIGA: -Borussia Dortmund Jana ndani ya Signal-Iduna-Park walilipa kisasi cha Msimu uliopita kufungwa 4-1 na Hamburg na kuibamiza Hamburg Bao 6-2 katika Mechi ya Bundesliga.

Bao za Borussia Dortmund zilifungwa na Robert Lewandowski na Pierre-Emerick Aubameyang, Bao 2 kila mmoja, Marco Reus na Mkhitaryan, Bao 1 kila mmoja.

Bao za Hamburg zilifungwa na Zhi Gin Lam na Heiko Westermann.

Mapema hiyo Jana, Mabingwa Watetezi Bayern Munich waliichapa Hannover Bao 2-0 na Bao zao kufungwa na Franck Ribey na Mandzukic.

Kwenye Bundesliga, Borussia Dortmund wanabaki kileleni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad