Taswira ya Sehemu ya pili ya mzunguko wa kwanza wa hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa michezo Nane. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 19, 2013

Taswira ya Sehemu ya pili ya mzunguko wa kwanza wa hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa michezo Nane.

CHELSEA:- Mechi nne bila ushindi. Kama Rafa Benitez angekuwa bado yupo kazini, anerushiwa mayai viza.
Jose Mourinho amepata kipigo katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa baada ya Chelsea kuchapwa mabao 2-1 nyumbani na FC Basle kwenye mchezo wa mashindano ya UEFA 2013/2014.

Ujumbe kwa kocha: Shabiki la Chelsea akipeleka ujumbe kwa kocha Mourinho kwamba Juan Mata anastahili kucheza na si kukaa benchi.

Oscar alitangulia kuwafungia The Blues dakika ya 45, lakini Salah akasawazisha dakika ya 71, kabla ya Streller kufunga la ushindi dakika ya 82 Uwanja wa Stamford Bridge.

Wachezaji Gary Cahill, Oscar na John Obi Mikel wakionekana wanyonge wakati Basle wanashangilia ushindi wao Stamford Bridge.

Marco Streller (wa pili kushoto) akiifungia bao la ushindi Basle jana (Septemba 18,2013) katika uwanja wa Stamford Bridge katika Mashindano ya UEFA 2013/2014.

Streller (katikati kushoto) akishangilia na mfungaji mwenzake Mohamed Salah.

Nahodha wa klabu, John Terry alisugua benchi.

ARSENAL:- imeanza vyema Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushinda ugenini mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Marseille Uwanja wa Velodrome, Ufaransa.
Mabao ya Gunners yalifungwa na Theo Walcott dakika ya 65 na Aaron Ramsey dakika ya 83, wakati la wenyeji lilifungwa na Jordan Ayew kwa penalti dakika ya 90.

Aaron Ramsey amefunga bao la sita msimu huu akiwa na Arsenal na hapa dakika ya 83 akiwapa ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji Marseille Uwanja wa Velodrome, Ufaransa.

Arsenal walifikiri walistahili kupewa penalti baada ya buti hili alilopigwa Per Mertesacker.

Rekodi ya klabu: Arsenal imetweet mechi zake 10 ilizoshinda ugenini

FC BARCELONA:- Lionel Messi amejibu mapigo ya mpinzani wake, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid baada ya kuifungia hat-trick FC Barcelona katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Ajax katika mchezo wa Kundi H wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uwanja wa Nou Camp.
Muargentina huyo pamoja na kufunga mabao matatu peke yake usiku, pia alitengeneza bao la nne lililofungwa na Gerard Pique.
Haikuwa bahati yao, Ajax kwani walikosa hadi penalti baada ya kipa Victor Valdes kuokoa mkwaju wa Kolbeinn Sigthorsson.
Messi alifunga mabao yake katika dakika za 22, 55 na 75, wakati Pique alifunga dakika ya 69.

Muargentina huyo Messi akifunga bao lake la pili katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Ajax katika mchezo wa Kundi H wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uwanja wa Nou Camp.

AC MILAN:- Christian Zapata akitimka kushangilia baada ya kuifungia bao la kwanza AC Milan dhidi ya Celtic.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, AC Milan iliichapa Celtic 2-0 Uwanja wa San Siro, mabao ya Zapata dakika ya 82 na Muntari dakika ya 85.

Wachezaji wa AC Milan wakiwa wameweka ukutawakati beki wa kati wa Celtic, Charlie Mulgrew akipiga mpira wa adhabu.

Sulley Muntari wa Milan akishangilia baada ya kufunga bao la pili zikiwa zimebaki dakika tano.

Mchezaji Phillipe Mexes akimrukia Cristian Zapata baada ya Mcolombia kufunga kwa AC Milan iliichapa Celtic 2-0.
Sehemu ya pili ya mzunguko wa kwanza wa hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya imeendelea usiku wa jana (Septemba 18,2013) kwa michezo nane iliyopigwa kwenye miji mikuu ya soka barani humo .

Kwenye uwanja wa Nou Camp Fc Barcelona waliwafunga Ajax Amsterdam 4-1 huku Lioneln Messi akiwa nyota wa mchezo baada ya kumjibu Cristiano Ronaldo kwa kufunga mabao matatu pekee yake . Bao lingine la mchezo huo lilifungwa na beki Gerrard Pique .

Jijini Milan kwenye uwanja wa Giuseppe De Meazza Ac Milan walipata ushindi wa tabu wakiwafunga Glasgow Celtic 2-0 . Wafungaji wa Milan kwenye mchezo huo walikuwa Sulley Muntari na Cristian Zappata.

Katika matokeo yaliyoshangaza wengi usiku wa jana (Jumatano) (Septemba 18,2013) mabingwa wa zamani wa amshindano haya Chelsea The Blues walipoteza mchezo wao dhidi ya Fc Basle tena kwenye uwanja wao wa nyumbani Stamford Bridge . 

Basle walishinda kwa mabao mawili kwa moja wafungaji wakiwa Marco Streller na Mohamed Salah huku Chelsea wakifunga kupitia kwa Oscar.

Arsenal waliendeleza mwanzo mzuri kwa timu za England kwenye msimu huu wa ligi ya mabingwa baada ya kuwafunga Olympique Marseille kwa mabao mawili kwa moja .

Mabo ya Arsenal yalifungwa na Theo Walcott na Aaron Ramsey huku Marseile wakifunga kupitia kwa Jordan Ayew ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati.

Mechi iliyokuwa inatazamiwa na wengi kuwa mechi ngumu pengine kuliko mechi zote za jana iliwakutanisha washindi wa pili wa ligi za Italia na Bundesliga Napoli na Borrusia Dortmund .

Katika mchezo huo uliopigwa huko Italia Napoli walishinda kwa mabao mawili kwa moja. Wafungaji wa Napoli walikuwa Gonzalo Higuain na Lorenzo Insigne huku Camilo Zuniga wa Napoli akijifunga mwenyewe kuipa Dortmund bao pekee lao mchezo huo .

Timu nyingine toka Hispania Atletico Madrid ilishinda mchezo wao dhidi ya Zenith St Petesburg kwa matokeo ya 3-1 huku Schalke 04 nao wakishinda mchezo wao dhidi ya Steua Bucharest kwa 3-0 . Nao Fc Porto waliwafunga Austria Wien 1-0.

Matokeo ya UEFA Champions League Septemba 18,2013.

Fc Barcelona 4-0 Ajax Amsterdam.

AC Milan 2-0 Glasgow Celtic .

Napoli 2-1 Borrusia Dortmund.

Marseile 1-2 Arsenal.

Chelsea 1-2 FC Basle.

Atletico Madrid 3-1 Zenith St Petersburg.

Austria Vienna 0-1 Fc Porto.

Schalke 04 3-0 Steua Buchares


Mechi zifuatazo ni za Hatua ya Pili ya Makundi UEFA 2013/2014:-Jumanne 1 Oktoba 2013.

FC Basel 1893 v FC Schalke 04

FC Steaua BucureÅŸti v Chelsea FC

Borussia Dortmund v Olympique de Marseille

Arsenal FC v SSC Napoli

Football Club Zenit v FK Austria Wien

FC Porto Club v Atlético de Madrid

AFC Ajax v AC Milan

Celtic FC v FC Barcelona

Jumatano 2 Oktoba 2013.

FC Shakhtar Donetsk v Manchester United FC

Bayer 04 Leverkusen v Real Sociedad de Fútbol

Juventus v Galatasaray A.Åž.

Real Madrid CF FC København

Paris Saint-Germain v SL Benfica

RSC Anderlecht v Olympiacos FC

Manchester City FC v FC Bayern München


PFC CSKA Moskva v FC Viktoria Plzeň

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad